• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

"Iringa changamkieni fursa jijini Dodoma" – Katibu Tawala Seneda

Imewekwa tarehe: December 7th, 2020

KATIBU Tawala Mkoa wa Iringa, Happiness Seneda ameitaka timu yake ya menejimenti kuchangamkia fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambalo ni Makao Makuu ya nchi ili kuchangia katika ukuaji wa uchumi wa taifa.

Kauli hiyo aliitoa katika kikao cha Menejimenti cha Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa ofisi hiyo mwishoni mwa wiki.

Seneda alisema kuwa amewakaribisha wataalam wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma katika kikao cha Menejimenti ili kuelezea fursa zilizopo jijini Dodoma.  

“Serikali imefanya maamuzi mazuri kuhamishia Makao Makuu Dodoma kwa sababu kumefungua fursa nyingi ambazo hazikuwepo awali. Na sisi tunataka kunufaika na fursa hizo, wawekezaji wa kwanza ni sisi” alisema Seneda. Timu ya wataalam wataelezea fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma na kuwashawishi kuzichangamkia, aliongeza.

“Ndugu zangu hakikisheni mnawekeza Dodoma, hamtajutia sababu fursa nyingi zipo wazi. Unapofanya uwekezaji jijini Dodoma maana yake, wewe unakwenda kutengeneza Masaki ya Dodoma na Posta ya Dodoma. Usije kuona kuwa Dodoma ni mbali, muda mfupi ujao utakuja kujutia. Mfano eneo la Nzuguni litakuja kupaa sana, uwanja wa mpira utajengwa hapo, Kituo Kikuu cha Mabasi kipo Nzuguni, Soko Kuu la Job Ndugai lipo Nzuguni hilo ni eneo la kimkakati,” alisema Seneda.

Kwa apande wake Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Zainab Manyike alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina fursa nyingi za uwekezaji.

“Halmashauri imetenga maeneo kwa ajili ya ujenzi wa viwanda mbalimbali katika Kata ya Nala. Eneo la Nala linapatikana barabara kuu ya kwenda Singida umbali wa kilometa 15 kutoka katikati ya Jiji. Eneo hili ni la kimkakati kwa ajili ya viwanda vya aina mbalimbali vikubwa na vidogo” alisema Manyike.

Akifafanua zaidi alisema kuwa maeneo yaliyotengwa ni kwa ajili ya viwanda vya kufua umeme wa upepo, matengenezo ya magari, na viwanda vya Dawa. Vingine ni viwanda vya nguo, viwanda vya vyakula, viwanda vya chuma na viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya biashara.

Aliongeza kuwa Halmashauri hiyo imepima viwanja kwa ajili ya matumizi mbalimbali kama ujenzi wa hoteli na nyumba za kupangisha katika maeneo ya Mtumba, Iyumbu, Njedengwa na Kitelela. Fursa nyingine alizitaja kuwa ni ujenzi wa shule na vituo vya afya. “Wote tunafahamu kuwa Jiji linaendelea kukua kutokana na idadi ya watu kuongezeka hivyo kuna fursa za uwekezaji katika ujenzi wa shule kwa ajili ya huduma za elimu.

Vilevile, ujenzi wa vituo vya afya na hospitali kwa ajili ya huduma za matibabu. Viwanja kwa ajili ya matumizi ya shule na hospitali vinapatikana maeneo ya Mtumba, Kikombo, Chahwa na Nala” alisema Manyike.

Kiutawala Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina ukubwa wa kilometa za mraba 2,576, ikiwa na kata 41 na mitaa 222.


Afisa Maendeleo ya Jamii katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Zainab Manyike akiongea na Timu ya Menejimenti ya Mkoa wa Iringa kuhusu fursa za uwekezaji zilizopo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.