• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jaji Mkuu amuapisha Prof. Elisante kuwa Katibu wa Tume ya Mahakama

Imewekwa tarehe: September 10th, 2021

Na. Mary Gwera, Mahakama

Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Hamis Juma leo amemuapisha rasmi Mtendaji Mkuu mpya wa Mahakama ya Tanzania, Prof. Elisante Ole Gabriel kuwa Katibu wa Tume ya Utumishi wa Mahakama kufuatia kustaafu kwa aliyekuwa Katibu wa Tume hiyo, Bw. Mathias Kabunduguru ambaye naye katika hafla hiyo ameagwa rasmi.

Hafla hiyo fupi ya uapisho wa Katibu wa Tume imefanyika leo Septemba 10, 2021 katika Ofisi ndogo za Bunge zilizopo jijini Dar es Salaam huku hafla ikiwa imehudhuriwa na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Mhe. Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Makamishna wa Tume hiyo, Katibu Mstaafu, Naibu Katibu wa Tume hiyo pamoja na Watumishi wa Tume.

Akizungumza mara baada ya kuapishwa rasmi, Prof. Ole Gabriel alimuhakikishia Jaji Mkuu pamoja na Viongozi wote wa Mahakama kuwa atajitahidi kufanya kazi kwa pamoja na kwa ushirikiano (team work) kuhakikisha kuwa malengo yaliyowekwa na Mahakama pamoja na Tume yanafikiwa.

“Naomba niwahakikishie kuwa nitatumia nguvu zangu zote, uwezo wangu nilionao kuhakikisha kuwa tunafanya kazi kwa pamoja na kufikia matarajio tuliyo nayo hususani katika suala ya kutoa haki kwa wakati kwa wananchi,” alisema Profesa.

Awali, akizungumza katika hafla hiyo, Katibu Mstaafu wa Tume hiyo, Bw. Mathias Kabunduguru alimkaribisha Katibu mpya huku akimdokeza masuala kadhaa ambayo Tume inakabiliwa nayo ikiwa ni pamoja na upungufu wa Watumishi ambapo idadi ya Watumishi iliyopo kwa sasa ni 16 na mahitaji halisi ni Watumishi 34.

Hata hivyo, Prof. Ole Gabriel ameahidi kushughulikia suala hilo la upungufu wa Watumishi kwa kufanya taratibu stahiki ili kuongeza idadi ya watumishi wa Tume hiyo ili kuipa nguvu zaidi Tume yenye mamlaka makubwa kitaifa ya kuisimamia Mahakama nchini.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Jaji wa Mahakama ya Rufani ambaye pia ni Kamishna wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, Mhe. Dkt. Gerald Ndika, Jaji Kiongozi, Mhe. Dkt. Feleshi, Msajili Mkuu, Mhe. Wilbert Chuma na Naibu Katibu wa Tume, Bi. Enziel Mtei walimshukuru Bw. Kabundunguru kwa kufanya kazi kwa kushirikiana kipindi chote alichokuwa Mahakama na Tume vilevile walimkaribisha Katibu mpya wa Tume na kumuahidi kushirikiana nae bega kwa bega katika kutekeleza majukumu yake.

Kufanyika kwa tukio hili la uapisho ni kwa mujibu wa Sheria namba nne (4) ya mwaka 2011 ya Uendeshaji wa Mahakama kifungu cha 16 (ii) ambacho kinamtaka Jaji Mkuu wa Tanzania ambaye ndiye Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi wa Mahakama, kumuapisha Mtendaji Mkuu wa Mahakama kuwa Katibu wa Tume hiyo.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.