• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jamii iendelee kujiandaa na kujikinga na maafa - Dkt. Yonazi

Imewekwa tarehe: June 30th, 2023

KATIBU Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera, Bunge na Uratibu Dkt. Jim Yonazi ameitaka jamii kujiandaa kila wakati ili kujikinga na maafa.

Ameyasema hayo mapema Leo Juni 30, 2023 Jijini Dodoma katika hafla ya uzinduzi wa Jukwaa Shirikishi la Mawasiliano ya Kidijitali la Afya Moja,

Dkt. Yonazi alisema kuwa, Tanzania kama Nchi imepitia historia ya kukabiliwa na matukio ya maafa yatokanayo na majanga na milipuko ya magonjwa ya binadamu na Wanyama hivyo ipo haja ya kuwa na mipango ya kitaifa inayoratibiwa vyema kuwezesha kubaini viashiria na kushirikishana taarifa ili kuzuia maafa yanayoweza kutokea.

Pia alibainisha kuwa, ufuatiliaji wa matukio yanayoweza kuathiri afya ya binadamu, wanyama na mazingira unatakiwa kufanyika kwa ufanisi kwa kuzingatia dhana ya Afya Moja kwa kutekeleza Mpango Mkakati wa Taifa wa Afya Moja 2022 - 2023.

Dkt. Yonazi alisema, matukio hayo hutokea bila matarajio na huhitaji utambuzi wa mapema na kuchukua hatua za haraka za kukabili. “Tumejifunza kuwa ili kudhibiti matukio hayo, hatuna budi kuimarisha mifumo ya tahadhari ya mapema na uratibu ili kudhibiti viashiria vya matukio yanayoweza kusababisha maafa kwa wakati.” Alisisitiza.

Aidha, Dkt. Yonazi alitumia fursa hiyo kuhimiza watendaji kujifunza kutoka kwa Nchi zilizoendelea katika mifumo ya aina hiyo kwa lengo la kuboresha masuala ya menejimenti ya maafa.

“Nimefurahi sana kuona kuwa kuna washiriki kutoka katika Wizara na Taasisi mbalimbali za Serikali,na wawakilishi wa vyombo vya Ulinzi na Usalama, na kwa kuwa hili ni toleo la kwanza, sasa nitoe wito kwa vyombo vya ulinzi na usalama, kuwa katika nchi zote zilizoendelea hawa ndio wabeba mwenge wa Sayansi na Teknolojia, tafiti zinafanywa katika majeshi na baada ya hapo huamishwa na hupelekwa katika matumizi mengineyo.” Alibainisha Dkt. Yonazi.

Sambamba na hilo alitoa wito kwa Vyuo vya Elimu ya Juu hususan Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kuendelea kutoa ushirikiano katika mtazamo wa kisayansi katika mambo yanayotatiza jamii na kuyatafutia ufumbuzi.

Kwa upande wake Mkuu wa Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) Profesa Raphael Chibunda alisema mradi huo wa kuanzishwa kwa  jukwaa shirikishi la kidijitali ulizunduliwa mwaka 2022,na kupitia mradi huu shughuli mbali mbali zimetekelezwa,na ili kuhakikisha kituo hiki kinafanya kazi kama ilivyokusudiwa ambapo Chuo cha SUA kilitoa vifaa vya TEHAMA vya Mradi huo vyenye thamani ya shilingi milioni 42.3.

Awali akitoa taarifa ya Mradi huo, Afisa TEHAMA kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu Bw. Alex Ndimbo alisema lengo la kuanzishwa kwa jukwaa hili ni kuongeza wigo kwa Jamii kutoa taarifa kwa mamlaka husika.

“Jukwaa hili linawakutanisha wataalam wote ambao wanasimamia sekta zinazohusiana na wanyama, binadamu na mazingira wakikutana pamoja na kuratibu tutapunguza matukio ambayo yataleta majanga katika Taifa letu, mfumo huu unaenda kuruhusu wananchi wa kawaida kabisa kutoa taarifa kwa Serikali au Idara husika moja kwa moja kutoka katika eneo la tukio kupitia namba 190 kwa baadhi ya mitandao ya simu,” Alieleza.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.