Na. Dennis Gondwe, DODOMA
MPANGO na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024 kujenga ukumbi wa kisasa wenye uwezo wa kuchukua watu 1,200 ili kutoa huduma ya kumbi na kuwaondolea usumbufu wakazi wa jiji.
Kauli hiyo ilitolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru alipokuwa akielezea vipaumbele vya Mpango na Bajeti ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa mwaka wa fedha 2023/2024.
Mafuru alisema kuwa Halmashauri ya Jiji imepanga kujenga ukumbi mkubwa wa kisasa. “Eneo lingine ni kujenga kumbi nyingine ya kisasa ya kuchukua watu 1,000 hadi 1,2000 kwa gharama ya shilingi 1,200,000,000 hadi 1,500,000,000. Hapa halmashauri ya Jiji la Dodoma bado tunapokea maombi mengi ya kumbi” alisema Mafuru.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.