• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji la Dodoma laibuka kinara Maonesho ya Nanenane 2019

Imewekwa tarehe: August 8th, 2019

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeibuka mshindi wa kwanza kwa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma katika Maonesho ya Nanenane mwaka 2019 na kuzawadiwa cheti na mgeni rasmi katika sherehe za kufunga maonesho hayo zilizofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni jijini hapa.

Akikabidhi cheti hicho, mgeni rasmi katika sherehe za kufunga maonesho hayo, Mkuu wa Mkoa wa Singida, Canon Dkt. Rehema Nchimbi alisema kuwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma imekuwa mshindi wa kwanza kwa upande wa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma. Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri ni Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa iliyoshika nafasi ya pili na Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa iliyoshika nafasi ya tatu.

Akiongelea ushindi huo, Afisa Kilimo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Agnes Woisso alisema kuwa ushindi huo ulitokana na maandalizi yaliyofanywa na Halmashauri hiyo. “Kulingana na vigezo vilivyowekwa na waandaaji, nadhani tulijitahidi kukidhi vigezo hivyo. Mfano tulikuwa na vipando (bustani) kwa njia mbalimbali, tulitumia viroba, makopo na bustani kichuguu  kama bustani za nyumbani na bustani za kawaida” alisema Woisso.  

Aliongeza kuwa banda la Jiji lilikuwa na wajasiriamali waliokuwa wakielezea kwa ufanisi shughuli zao kulingana na kaulimbiu na Nanenane mwaka huu 2019. Maeneo mengine ya kimkakati ni mabango safi, upambaji wa mabanda safi na sare kwa watoa huduma katika mabanda safi, aliongeza.

Kwa upande wa mifugo, alisema kuwa Halmashauri ilikuwa na ng’ombe wa maziwa wenye viwango bora, kuku wa mayai, sungura na mbuzi, mambo yaliyowavuta watu wengi kwenda kujifunza.

Maonesho ya 26 ya Nanenane yaliyofanyika katika viwanja vya Nanenane Nzuguni Dodoma yalishirikisha makampuni 36, wajasiriamali 300 na taasisi 43 yakiongozwa na kaulimbiu isemayo “Kilimo, mifugo na uvuvi kwa ukuaji wa uchumi wa nchi”.

Mgeni rasmi wa kilele cha Maonesho ya Nanenane Kanda ya Kati 2019 Canon Dkt. Rehema Nchimbi ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Singida akiwapungia mikono wananchi na washiriki wa maonesho ya Nanenane kuonesha furaha yake, kulia kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge.


Mkuu wa Mkoa wa Singida Canon Dkt. Rehema Nchimbi (aliyeshika cheti) akisamiliana na Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Baltazari Ngowi kabla ya kumkabidhi cheti cha ushindi wa kwanza wa Maonesho ya Nanenane kwa Halmashauri za Mkoa wa Dodoma, maonesho haya yalifanyika kwenye viwanja vya Nanenane Nzuguni Dodoma na kufikia kilele chake tarehe 08/08/209.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.