• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

JIJI LA DODOMA LAZINDUA ZOEZI LA UBAINISHAJI WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Imewekwa tarehe: December 5th, 2023

Na. Dennis Gondwe, HOMBOLO BWAWANI

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imezindua zoezi la ubainishaji watoto wenye mahitaji maalum katika jamii ili waweze kupata haki yao ya elimu na matunzo kwa mujibu wa sheria.

Kauli hiyo ilitolewa na Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Issa Kambi alipokuwa akizindua zoezi la ubainishaji watoto wenye mahitaji maalum katika jamii uzinduzi uliofanyika katika Shule ya Msingi Hombolo Bwawani iliyopo Kata ya hombolo Bwawani jijini Dodoma.

Kambi ambae ni Afisa Elimu Maalum katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma alisema “kwa niaba ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ambae alipenda sana kuwa nasi hapa leo napenda kuzindua rasmi zoezi la ubainishaji watoto wenye mahitaji maalum kwa maana ya kwenda kuwatafuta mtaani na kuwaleta kwenye vituo vyetu kama hiki na vitengo vingine. Zoezi litafanyika katika mitaa nane ya Itega, Salama, Lugala, Mnyakongo, Mtube, Nala, Chigongwe na Mbalawala”.

Alisema kuwa lengo la zoezi hilo ni kuwabaini watoto hao mahali walipo na kuwasogeza kwenye huduma na kuwapatia afua stahiki ikiwa ni pamoja na elimu na matunzo. “Tunafahamu kwamba baadhi ya familia zinaamini watoto hawa hawawezi kufanya mambo, lakini tunapokwenda kufanya ubainishaji tunawatia moyo na kuwashawishi kuwaleta watoto hawa shule. Kuanzia ngazi za familia tunapeleka elimu na baadae tunawaleta kwenye vituo kama hivi na kama mlivyoona watoto hawa wanafuraha” alisema Kambi.

Akiongelea umuhimu wa zoezi hilo, Mkazi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma Juliana Linus alisema kuwa zoezi hilo ni muhimu kwa sababu linakwenda kuwapatia haki ya msingi watoto wenye mahitaji maalum katika Jiji la Dodoma. “Ni kweli wapo baadhi ya wazazi ambao wamekuwa na tabia ya kuwaficha watoto wao wenye ulemavu jambo linalowanyika haki watoto hao kupata elimu, afya na malezi bora” alisema Linus.

Zoezi la uzinduzi wa ubainishaji watoto wenye mahitaji maalumu katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilihudhuriwa na Jumuiya ya Shule ya Msingi Hombolo Bwawani ambayo ni shule jumuishi, Diwani wa Kata ya Hombolo Bwawani, maafisa waandamizi kutoka Halmashauri ya Jiji la Dodoma na wawakilishi wa Jumuiya ya Shule ya Msingi Feza tawi la Dodoma na wawakilishi wa serikali ya mtaa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.