• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji la Dodoma linafursa lukuki uwekezaji

Imewekwa tarehe: October 26th, 2024

Na. Faraja Mbise, DODOMA

HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma inazo fursa lukuki kwa ajili ya wawekezaji na wafanyabiashara katika maeneo ya kilimo, viwanda, biashara, michezo na maeneo mengine yanayoweza kusisimua ukuaji wa uchumi.

Kauli hiyo ilitolewa na Kaimu Mkuu wa Divisheni ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Abdul Chacha alipokuwa akizungumza na wajumbe wa Mkutano wa Baraza la Biashara Wilaya ya Dodoma uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma uliopo Mji wa Serikali Mtumba. “Halmashauri ya Jiji la Dodoma ina fursa nyingi sana, una fursa ya kuwekeza katika maeneo ya michezo kwa ujumla, kwasababu saizi tunaangalia AFCON inakuja. Kwahiyo, watu wengi watahitaji sehemu ambazo zimeandaliwa kwa ajili ya michezo. Vilevile, nyumba za kupanga na kuuza (apartments). Kipindi hiki wageni wanaingia wengi sana hivyo, wanahitaji sehemu za kufikia kwa maana ya malazi, hizo ni fursa zinazopatina. Lakini biashara mbalimbali za chakula kama kuku, nyama, mbogamboga na matunda ni mahitaji katika soko la Jiji la Dodoma. Sasa hivi, mtaona magari mengi ambayo yalikuwa yanatoka mikoani yanaenda Dar-es-Salaam yanashusha bidhaa zao hapa Dodoma. Kwahiyo, hata mzunguko wa pesa umeongezeka mara dufu tofauti na ilivyokuwa zamani” alisema Chacha.

Akiongelea utatuzi wa changamoto, alisema kuwa baraza hilo limekuwa msaada mkubwa. “Changamoto nyingi tumeweza kuzitatua. Mfano, wafanyabiashara wanalalamika kuhusu ushuru au kodi zilizowekwa ambazo hawazifahamu, lakini baada ya kukutana nao katika vikao vyetu, tunawafahamisha zile kodi zimewekwa kwa utaratibu gani, malengo yake ni yapi. Wafanyabiashara wamekuwa wakielewa na utaratibu unaendelea. Pia changamoto nyingine tuna wafanyabiashara wadogo na wa kati, wafanyabiashara wadogo mfano machinga wanachangamoto ya maeneo ya kufanyia biashara. Hivyo, tunakaa nao na kuongea na kukubaliana mambo ya msingi. Baraza hili kupitia halmashauri wataandaliwa maeneo maalumu ambayo utaona wanapewa yakiwa na huduma zote za msingi ili waweze kutoa huduma zao” aliongeza Chacha.

Akiongelea ujio wa reli ya kisasa (SGR) alisema kuwa imesaidia kukuza biashara katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Kitakwimu bado tunaendelea kufanya tafiti zetu, lakini kiwango kikubwa sana mtaona ‘movement’ ya watu kwenda Dar-es-Salaam na kurudi ni kubwa zaidi. Hii imefanya biashara katika Jiji la Dodoma isiwe na tofauti kubwa na ile iliyopo katika Jiji la Dar-es-Salaam kwasababu zinapatikana kwa wepesi na gharama nafuu kwasababu wafanyabiashara hawatumii muda mrefu sana kufuata bidhaa zao” alisisitiza Chacha.

Kaimu mkuu huyo wa Divisheni ya Uwekezaji, Viwanda na Biashara aliwataka wafanyabiashara na watanzania kwa ujumla kulipa kodi kwa uaminifu ili kuleta maendeleo katika nchi. “Tumeendelea kuwaelimisha na kuwahamasisha watanzania kwa ujumla kwamba kodi zao ndio zinazojenga nchi, upatikanaji wa kodi zao ndio unaofanya maendeleo yote yanayoonekana sasahivi yanatokana na kodi zao. SGR ni kodi zao, miundombinu, barabara, huduma za kijamii, huduma za afya zote zinaweza kufanyika kwasababu ya kodi zao. Kwahiyo, mchango wa kodi ya wananchi ni muhimu sana kwa maendeleo” alisisitiza Chacha.

Nae mkazi wa Kikuyu Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Jema Wenslaus alisema kuwa ujio wa treni ya SGR umeyafanya maisha kuwa rahisi zaidi. Alisema kuwa awali alikuwa akipanga safari ya kutoka Dodoma kwenda Dar es Salaam na kuipangua kutokana na muda wa kusafiri kuwa mrefu. “Baada ya kuanza kwa SGR sasa unaweza kwenda na kurudi siku hiyohiyo tena bila kuchoka. Treni hii hakika inaokoa muda na imerahisisha maisha” alisema Wenslaus.

Baraza la Biashara la Wilaya ya Dodoma linahusisha wafanyabiashara kutoka sekta ya umma na sekta binafsi kwa lengo la kujadili masuala ya biashara na uwekezaji kwa mapana, changamoto na utatuzi wake, muelekeo na namna ya kufikia maelengo ya halmashauri, wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla.




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.