Na. Dennis Gondwe, DODOMA
HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeanzisha teknolojia ya nishati mbadala ili kuondoa matumizi ya kuni na mkaa kwa wakazi wa mikoa ya kanda ya kati.
Kauli hiyo ilitolewa na Afisa Mifugo katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma, George Joram alipokuwa akiongelea teknolojia ya nishati mbadala inayooneshwa katika banda la mifugo Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Joram alisema “safari hii tumekuja na teknolojia ya nishati mbadala. Tunazalisha gesi kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe. Kinyesi cha ng’ombe tunakikusanya kutoka kwenye banda la ng’ombe tunachanganya kwa mchanganyo wa moja kwa moja. Tunachukua kinyesi cha ng’ombe kwenye ndoo ya lita 20 na maji lita 20 tunachanganya na kuzalisha gesi”.
Alisema kuwa baada ya saa 24 bacteria wanazalisha gesi inayoitwa Methane. “Badala ya kutumia mkaa na nishati nyingine kama kuni, unaweza kutumia nishati mbadala ya kutumia gesi ya kinyesi cha mifugo na kulinda na kutunza mazingira. Karibuni sana Banda la Mifugo la Halmashauri ya Jiji la Dodoma mjionee wenyewe mambo ni motomoto” alisema Joram kwa furaha
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.