Na. Dennis Gondwe, DODOMA
KATA ya Zuzu imempongeza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru kwa kutekeleza vizuri Ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) jambo linalowafanya wananchi kuiunga mkono serikali yao.
Kauli hiyo ilitolewa na Diwani wa Kata ya Zuzu, Awadhi Abdallah alipokuwa akielezea jinsi kata yake inavyonufaika na utekelezaji wa miradi.
Abdallah alisema “nichukue nafasi hii kumshuuru na kumpongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru kwa kutekeleza Ilani ya CCM. Kata ya Zuzu yale tuliyoahidi tunayatekeleza na wananchi wanaunga mkono juhudi za serikali yao”.
Diwani huo alipongeza mpango wa halmashauri wa kuziboresha shule za msingi. “Mkurugenzi amekuja na mpango mkakati mzuri wa kuhakikisha shule za msingi zinakwenda kukamilisha upungufu wa madarasa, upungufu wa madawati na upungufu wa walimu katika Jiji la Dodoma. Kwa maana hiyo, Kata ya Zuzu inanufaika na kutekelezezwa kwa Ilani ya CCM” alisema Abdallah.
Akiongelea madarasa kwa elimu ya sekondari, alisema kuwa yanajitosheleza. “Sisi Kata ya Zuzu tunamshukuru sana Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutukumbuka kwenye madarasa ya sekondari. Kata ya Zuzu hatuna upungufu wa madarasa ya sekondari kwa idadi ya wanafunzi tulionao sasa” alisema Abdallah.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.