HALMASHAURI ya Jiji la Dodoma imeendelea kushiriki katika maonesho ya Wiki ya Sheria yanayoendelea katika viwanja vya Nyerere Jijini humo ambapo wadau wadau mbalimbali wamekuwa wakipatiwa elimu ya huduma zinazotolewa na jiji hilo ikiwemo umiliki wa ardhi na sheria zake.
Wataalam wa idara mbalimbali za Jiji hilo ikiwemo Ardhi na Mipango Miji, Sheria, na Mipango na Ufuatiliaji wanatumia fursa ya maonesho hayo kutoa elimu katika banda la jiji hilo huku baadhi ya wadau waliotembelea eneo hilo wakipongeza huduma zinazotolewa.
Maonesho hayo ya Wiki ya Sheria yalifunguliwa hivi karibuni na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Hussein Mwinyi na yanatarajiwa kufungwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwenye viwanja vya Chinangali jijini humo.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.