• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Jiji, wadau kusimamia mipango miji

Imewekwa tarehe: June 9th, 2021

WIZARA ya Ardhi, Nyumba na Mendeleo ya Makazi, Mamlaka ya Viwanja vya Ndege nchini (TAA), Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TCAA), na Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, wamekubaliana kuja na mwarobaini wa kuondoa kero za matumizi ya ardhi kwa wakazi na wawekezaji wanaojenga maeneo karibu na viwanja vya ndege nchini.

Mpango huo umetangazwa hivi karibuni na wawakilishi wa taasisi hizo waliposhiriki warsha ya siku moja ya mipango endelevu ya matumizi bora ya ardhi yanayoenda sambamba na uendeshaji wa viwanja vya ndege nchini, iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Kiwanja cha Ndege cha Dodoma.

Mkuu wa Kitengo cha Mazingira cha TAA, Maxmilian Mahangila amesema warsha hiyo ina lengo la kuweka sheria sawa kati ya sheria za ardhi, mipango miji pamoja na sheria za masuala ya usalama wa anga, ambapo zimekuwa zikitofautiana kutoka kwenye taasisi moja na kwenda nyingine.

“Ukiangalia hizi sheria zimekuwa zikisigana bila kujua, ambapo ukiangalia sheria zilizowekwa za masuala ya anga zinakataza ujenzi wa majengo marefu, minara na makazi karibu na viwanja vya ndege, lakini sheria za ardhi na hata mipango jiji zinaruhusu ujenzi wa aina yeyote katika maeneo hayo, ambapo hutoa kibali kwa wazawa au wawekezaji kujenga bila tatizo,” amesema.

Hata hivyo, amesema wadau mbalimbali wametoa ushauri juu ya matumizi ya sheria hizo ili ziwe na mtazamo mmoja, ukizingatia sheria na kanuni za masuala ya anga ili kuepusha madhara yanayoweza kusababishwa kwa kutokuwa na mpango bora wa matumizi ya ardhi.   

Warsha hiyo ilikuwa na mada tatu, ambazo ni “Mipango ya Matumizi ya ardhi yanayoenda sambamba na uchafuzi wa mazingira” iliyowasilishwa na Joyce Kasebele, Afisa Mazingira wa TAA, ambapo amezungumzia mazao yanayoweza kulimwa maeneo yanayozunguka viwanja vya ndege, ambayo hayavutii ndege hai.

Pia amezungumzia  jinsi wananchi wanaoishi maeneo ya kuzunguka viwanja hivyo kuhakikisha wanayaweka katika hali ya usafi, ili kuepusha wanyama na ndege hai kuingia na kufanya madhara kwenye ndege za abiria na mali nyingine.

Naye Meneja wa TCAA wa mkoa wa Dodoma, Ludovic Ndumbaro aliyewasilisha mada ya “Sheria na kanuni za masuala ya anga kuhusiana na matumizi ya ardhi yanayozunguka viwanja vya ndege nchini”.

“Majengo marefu ni hatarishi karibu na viwanja vya ndege, na kila anayejenga maeneo hayo lazima apate kibali maalum kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa TCAA, baada ya kujiridhisha kama halina madhara ataruhusiwa lakini yale yenye madhara hayawezi kuruhusiwa kwani yanaweza kuzuia ndege wakati wa kupaa na kutua,” amesema Ndumbaro.

Halikadhalika Afisa Mipango Miji Mwandamizi wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Edward Mpanda aliyewasilisha mada ya “Mpango wa matumizi ya Ardhi” amesema ndani ya wizara na katika ngazi za wilaya mipango ya matumizi ya ardhi yamezingatia maeneo ya viwanja vya ndege.

“Pamoja na kwamba hizi sheria na mipango ipo wazi kuanzia ngazi ya wilaya na wizarani, lakini imeshughudiwa baadhi ya viwanja vya ndege vimekuwa sio salama kutokana na matumizi mabaya ya ardhi kutoka kwa wananchi wanaozunguka eneo hilo kuhakikisha majengo yao yanakuwa na urefu wa kawaida ili kuondoa vizuizi vya wakati wa kutua na kuruka kwa ndege,” amesema Mpanda.

Naye Mpima Ardhi Jiji la Dodoma, Hudson Magomba amesema kwa upande wa mpango jiji kumekuwa na mpango wa muda mrefu kuhusuana na  viwanja vya ndege wa mwaka 2010 na baadae kufanyiwa maboresho mwaka 2019-2039.

Hatahivyo, amewataka wananchi kufuata taratibu za ujenzi na kujenga maeneo yaliyopimwa na serikali, na wasivamie maeneo ya viwanja vya ndege kwani ni hatarishi kwa maisha yao.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.