NAIBU Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Mwanaidi Khamis ameitaka jamii kutokukaa kimya na kunyamazia vitendo vya ukatili vinavyotokea ili kuwa na Jamii iliyo salama hasa kwa Wanawake na Watoto.
Aliyasema hayo wakati wa ziara yake mkoani Geita iliyolenga kufuatilia utekelezaji wa sera na mipango mbalimbali ya wizara katika Mamlaka ya Mikoa na Serikali za Mitaa nchini.
"Nimefika katika Mkoa huu wa Geita nimepokea taarifa ya Mkoa nimeona masuala ya ukatili dhidi ya wanawake na watoto yameshamiri, jumla ya mashauri 625 kwa watu wazima na mashauri 133 ya vitendo dhidi ya watoto yameripotiwa, sasa tusikae kimya tupaze sauti tutokomeze ukatili." Alisema Khamis
Aidha, aliwataka Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii kuwasikiliza wananchi katika maeneo yao ili kuwasaidia kutatua changamoto mbalimbali wanazokabilia nazo katika jamii hasa za upatikitanaji wa fursa za kiuchumi na ukatili wa kijinsia.
"Ndugu zangu Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii Rais Samia Suluhu Hassan ameiunda Wizara hii muhimu mtusaidie kuwafikia wananchi kutatua changamoto zao, tuwasaidie wananchi tuwasikilize." Alisisitiza Khamis
Wakati huo huo alipokea taarifa ya Utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa kutokomeza ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto (MTAKUWWA) katika Kata ya Nyamigota na amewasihi wajumbe wa kamati ya MTAKUWWA kuhakikisha wanatoa elimu kwa jamii ili wawe na uwezo wa kutoa taarifa za vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto na kuilinda jamii.
"Ndugu zangu Maafisa Ustawi wa Jamii na Maendeleo ya Jamii Rais Samia Suluhu Hassan ameiunda Wizara hii muhimu mtusaidie kuwafikia wananchi kutatua changamoto zao, tuwasaidie wananchi tuwasikilize." Alisisitiza Khamis
Aidha, alitembelea Kikundi cha Manyuki Company Grading Rice killichopo Mamlaka ya Mji mdogo wa Katoro Halmashauri ya Wilaya ya Geita na kuwataka Wanawake kujiunga katika vikundi vya kiuchumi ili waweze kupata fursa mbalimbali za kupata mikopo kwaajili ya kupata mitaji na masoko ya bidhaa wanazozalisha katika vikundi vyao.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Geita, Karia Rajab Magaro alimuhakikishia Naibu Waziri, Mwanaidi Khamis kuratibu masuala yote ya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii na kuhakikisha Maafisa wa kada hizo wanawafikia wananchi kusikiliza na kutatua kero zao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.