Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo amekata utepe kuashiria uzinduzi wa Rada mbili za kuongozea Ndege ktk Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa J.K Nyerere na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa KIA katika Sherehe zilizofanyika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar.
Baadhi ya dondoo:
"Mradi huu umesaidia kuokoa fedha tulizokuwa tunalipa kwa nchi jirani, mradi utatuwezesha kutoa huduma kwa nchi jirani na kupata fedha. Rada hizi zina manufaa mtambuka ambayo yatagusa maeneo mengi".
"Hatuwezi kukubali kukwamishwa, sisi tutaendelea mpaka tufike pale tulipopanga kama nchi, tuna kiu ya maendeleo, tusikubali mtu yeyote atuchezee"
"Uwepo wa rada hizi utasaidia sana kulinda anga letu, hii ni hatua kubwa sana katika sekta ya anga. Mradi huu utaleta manufaa makubwa sana katika nchi yetu ikiwemo sekta ya usafiri wa anga".
"Ni lazima tufanye kazi, muda wa kubembelezana haupo tena, tumekabidhiwa madaraka na wananchi. Viongozi wenzangu tusimamie haya tuliyokabidhiwa na tusiwe kikwazo, tutatue kero za wananchi"
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.