• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

JPM azindua viwanda vikubwa 3 Morogoro

Imewekwa tarehe: February 12th, 2021

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 12 Februari, 2021 amezindua viwanda vikubwa 3 vilivyopo Mkoani Morogoro na ameagiza viongozi wa Wizara ya Viwanda na Biashara, Uwekezaji na Mamlaka za Serikali za Mitaa kuondoa urasimu unaokwamisha ujenzi wa viwanda hapa nchini.

Mhe. Rais Magufuli aliyekuwa katika ziara ya kikazi ya siku 2 Mkoani Morogoro, kwanza amezindua kiwanda cha Ngozi Taifa (Taifa Leather Company Limited) kilichowekezwa na Mtanzania Bw. Rostam Aziz kwa gharama ya takriban shilingi Bilioni 50.

Kiwanda hicho kikubwa zaidi Barani Afrika kina uwezo wa kuchakata vipande 4,000 vya Ngozi ya Wanyama wakubwa na vipande 1,0 vya ngozi ya wanyama wadogo kwa siku na kinatarajiwa kuongeza uzalishaji mwishoni mwa mwaka 2022 ambapo kitachakata vipande 5,000 vya ngozi ya wanyama wakubwa na vipande 15,000 vya ngozi za wanyama wadogo.

Baada ya kuzindua kiwanda hicho, Mhe. Rais Magufuli amempongeza Bw. Rostam Aziz kwa uwekezaji huo, ameiagiza Wizara ya Mifugo na Uvuvi kufanyia kazi maombi ya kuondoa kodi katika kemikali za kuchakatia Ngozi na ameagiza kuongezwa kwa kiwango cha kodi kutoka asilimia 80 hadi 100 kwa Ngozi zinazosafirishwa kwenda nje ya nchi zikiwa ghafi ili ngozi hizo ziweze kuchakatwa hapa hapa nchini ambapo zitaongeza ajira na mapato kwa Serikali.

Mhe. Rais Magufuli ameeleza kutofurahishwa na watu waliobinafsishwa viwanda na kisha kutoviendeleza akiwemo Mhe. Aziz Abood aliyebinafsishiwa viwanda vya mafuto ya mgando (Moproco Factory) na maturubai (Morogoro Canvas) na ameagiza Benki ya CRDB na Msajiri wa Hazina kuhakikisha viwanda hivyo vinagawiwa kwa wawekezaji wengine mara baada ya Mhe. Azis Abood kunyang’anywa.

Pili, Mhe. Rais Magufuli amezindua kiwanda cha kukoboa mpunga (Murzar Wilmar Rice Mills Ltd) kilichojengwa kwa gharama ya shilingi Bilioni 48 na ambacho kina uwezo wa kukoboa tani 288 za mpunga kwa siku na kisha kufungasha mchele katika ujazo na madaraja mbalimbali.

Kiwanda hicho kimeajiri wafanyakazi 75 na kinanunua mpunga kutoka kwa wakulima takribani 5,000 kutoka Mikoa ya Morogoro, Mbeya, Shinyanga na Tabora ambapo katika mwaka 2020 kimenunua tani 65,000 zenye thamani ya shilingi Bilioni 45.

Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni ya Murzar Wilmar Rice Mills Ltd kwa kuwekeza katika kiwanda hicho kikubwa kuliko vyote hapa nchini kwa kukoboa mpunga, ametoa wito wamiliki wake kuutambulisha mchele unaozalishwa kiwandani hapo  kwa majina ya Kitanzania badala ya jina linalotumika sasa na pia ameeleza kutofurahishwa na nchi kuendelea kuuza nje ya nchi mazao ambayo hayajasindikwa na kuongezwa thamani mfano mpunga badala ya mchele na mahindi badala ya unga.

Tatu, Mhe. Rais Magufuli amezindua kiwanda cha kusafisha na kufungasha mazao ya jamii ya kunde (choroko, mbaazi, dengu, pilipili manga, karafuu, ufuta, maharage na karanga) kilichojengwa na kampuni ya Mahashree Agro Processing Tanzania Limited katika eneo la Mikese kwa gharama ya shilingi Bilioni 25.

Mhe. Rais Magufuli ameipongeza kampuni hiyo kwa kuwekeza katika kiwanda ambacho kitawezesha wakulima wa mazao hayo kupata soko na ametoa wito kwa wawekezaji wengine wa ndani na nje ya Tanzania kuja kuwekeza hapa nchini kwa kuwa wawekezapo hapa watakuwa na uhakika wa soko la watu takribani Milioni 60 wa Tanzania, watu takribani Milioni 165 wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) na watu takribani Milioni 400 wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADS), ambazo zina makubaliano ya kuondoa vikwazo na kujenga mazingira mazuri ya ushirikiano wa biashara na uwekezaji.

Mhe. Rais Magufuli ameikaribisha kampuni ya Mahashree Agro Processing Tanzania Limited kuwekeza katika uzalishaji wa sukari kama ilivyoahidi na ametaka viongozi wanaohusika kuwezesha mpango huo kwa kuwa wazalishaji wa sukari hapa nchini hawajaongeza uzalishaji kama walivyoahidi.

Aidha, Mhe. Rais Magufuli amekubali ombi la Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Mhe. Hamis Taletale (Babu Tale) la kujengwa barabara ya lami ya Bigwa – Kisaki (km 78) ambapo ameiagiza Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi kutangaza zabuni ya kuanza ujenzi wa kilometa 40 za mwanzo kwa kuwa barabara hiyo ni muhimu kwa uchumi na ustawi wa wananchi wa Morogoro Kusini.

Mhe. Rais Magufuli amemaliza ziara yake ya siku 2 Mkoani Morogoro na ameingia Mkoani Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Loata Ole Sanare, Mkurugenzi wa Kiwanda cha Ngozi cha Taifa-Morogoro Rostam Aziz wakati akifungua Kiwanda hicho cha Ngozi cha Taifa-Morogoro kilichopo Kihonda katika Manispaa ya Morogoro.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia ngozi ambayo imeshatengenezwa kwenye Kiwanda cha Taifa kilichopo Morogoro.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiangalia moja ya bidhaa za mchele wa aina mbalimbali katika Kiwanda cha MW Rice Millers limited mara baada ya kukifungua rasmi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kufungua Kiwanda cha Kuchakata Mpunga cha MW Rice Millers limited kilichopo Kihonda mkoani Morogoro.

 

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.