UJUMBE wa Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Mohamed Mchengerwa ukiongozwa na Naibu Katibu Mkuu Wizara hiyo Bw. Saidi Yakubu wamekutana na kufanya kikao pamoja na Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Hussain Amhed.
Aidha, katika mazungumzo yao Naibu Katibu Bw. Yakubu ametumia fursa hiyo kumkaribisha Balozi wa Qatar hapa nchini Mhe. Hussain Amhed kushiriki kilele cha maadhimisho ya Siku ya Kiswahili Duniani ambayo yanaadhimishwa kwa mara ya kwanza duniani baada ya kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa 41 wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) Novemba 23, 2021 ulipitisha azimio namba 41C/61 la kutangaza tarehe 7 mwezi Julai kila mwaka kuwa Siku ya Kiswahili Duniani.
Katika maadhimisho hayo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi ambapo siku hiyo itaadhimishwa kuudhihirishia ulimwengu kuwa asili ya lugha ya Kiswahili ni Tanzania.
Kwa upande wake Balozi Mhe. Hussain amesema amepokea maombi hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kuzingatia uhusiano na ushirikiano mzuri uliyopo baina ya nchi hizo mbili.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.