• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kamati ya Bunge yafurahishwa na mradi wa hotel ya Jiji Dodoma

Imewekwa tarehe: August 22nd, 2023

Na. Dennis Gondwe, DODOMA

KAMATI ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imefurahishwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma kujenga hoteli kwa ajili ya kuongeza mapato na kutoa huduma bora kwa wananchi.

Kauli hiyo ilitolewa na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya LAAC, Stanslaus Mabula alipoongoza kamati hiyo kukagua miradi ya ya kimkakati katika Halmashauri ya Jiji la Dodoma.

Mabula ambae ni Mbunge wa Jimbo la Nyamagana alisema “kwanza niwapongeze sana Halmashauri ya Jiji la Dodoma kwa kufikiria kuwa na vitega uchumi ambavyo kiukweli vitaipaisha halmashauri hii. Kamati tumefurahishwa kuona kwanza ile hoteli ya Jiji la Dodoma ambayo tayari imepata mwendeshaji, sababu tunaamini halmashauri haiwezi kufanya kazi ya kuendesha hoteli vingenevyo itakuwa changamoto. Hiyo peke yake inawapa uhakika kwamba mradi mlionao tayari unawaingizia kipato. Sisi kama kamati tumekuwa na msisitizo kila wakati, kwanza kuhakikisha halmashauri zinaongeza mapato kwa kubuni vyanzo vingi zaidi ili ziweze kuongeza mapato mengi zaidi”.

Alisema kuwa imani ya kamati yake ni kuwa lengo kubwa la miradi ya uwekezaji wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma ni kulifanya jiji hilo liweze kujitegemea. ”…na majiji mengi bado hayana miradi ya namna hii. Dodoma ni Jiji changa lakini limekuja kwa kasi ya hali ya juu kwa hiyo tunawapongeza sana” alisema Mabula.

Akisoma taarifa ya mradi wa Hoteli ya Jiji la Dodoma (Best Western Dodoma City Hotel) Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, John Kayombo alisema kuwa hoteli hiyo ilijengwa kwa gharama ya shilingi 9,995,881,126.75. “Mradi huu umejumuisha miundombinu mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha utoaji wa huduma nzuri na za kisasa kwa wateja hali iliyofikia kuwa na hadhi ya nyota nne. Hoteli ina ghorofa 11, vyumba vya kulala 95 kati ya hivyo 63 ni vyumba vya kawaida ambavyo vinatumika. Vyumba vitatu ni ‘presidential suite’, kumbi tatu za mikutano migahawa mitatu, bwalo la kuogelea moja, chumba cha mazoezi, lifti tatu na eneo la maegesho ya magari” alisema Kayombo.

Akiongelea mafanikio ya mradi alisema kuwa ni kuongeza mapato kwa Halmashauri ya Jiji la Dodoma. “Faida nyingine ni kutoa huduma za kijamii kwa wananchi wa ndani na nje ya Jiji la Dodoma. Mradi umetoa fursa za ajira kwa wananchi ambapo hadi sasa jumla ya wananchi 80 wameajiriwa” aliongeza Kayombo.

Ikumbukwe kuwa mradi wa hoteli ya Halmashauri ya Jiji la Dodoma ulianza kujengwa Mwezi Agosti, 2019 na kukamilika Aprili, 2023.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.