• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kamati za Huduma za Afya Mkoa na Wilaya zatakiwa kuwa na Ubunifu

Imewekwa tarehe: March 15th, 2019

Kamati za huduma za afya Mkoa (RHMT) na Wilaya (CHMT) nchini zimetakiwa kuwa wabunifu katika kutekeleza shughuli zake na kuhakikisha wanaboresha huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi Mkoa kwa ujumla ili kuleta matokeo bora kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa na Naibu Katibu Mkuu Afya, Ofisi  ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dkt.Dorothy Gwajima katika kikao cha mrejesho wa utekelezaji wa yatokanayo na ziara za usimamizi shirikishi za utendaji kwa watoa huduma za afya katika Halmashauri ya Jiji  la Dodoma na Halmashauri ya Chamwino leo Jijini Dodoma kilichofanyika katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI.

Kikao hicho ni mwendelezo wa mkakati maalumu wa kuzifunda timu za uendeshaji huduma za afya Mikoa na Wilaya kwa kuanzia na Mkoa wa Dodoma ili,ziweze kufanya uwajibikaji wenye matokeo na kuwaridhisha watumiaji wa huduma za vituo vya tiba na kuwa mfano wa kuigwa na Mikoa mingine” be the center of excellence”.

Wajumbe wa Kamati ya huduma za afya Wilaya (CHMT) ya Jiji la Dodoma wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu Afya OR-TAMISEMI, Dkt.Dorothy Gwajima (hayupo pichani) alipotembelea Jiji la Dodoma na kujionea shughuli za Afya katika Jiji la Dodoma.

Dkt. Gwajima amesema kuwa, ubunifu unaotakiwa ni kujenga mahusiano mazuri baina ya mteja na mtoa huduma za afya ili, mteja aweze kuwa uhuru na kujisikia faraja katika kupata huduma kutoka kituoni hapo.

Amesema ni muhimu kuweka mkazo katika eneo la kitabibu na kuhakikisha kuwa, huduma hizo ni sahihi, salama na rafiki kwa vigezo vyote na wateja wanaridhika nazo.

“Mahusiano mazuri yanajengwa na ukarimu, lugha nzuri kwa mteja na umahiri wa utendaji kazi wenu wa kitaaluma kwa ujumla wakati wa kuwahudumia wateja wenu kwa kuwa wateja waliohudumiwa vizuri ndiyo ambao mawakili wazuri katika jamii yao kulingana na jinsi ambavyo wamefurahia huduma zenu” Amesema Dkt.Gwajima

Dkt.Gwajima amewaagiza  watoa huduma za afya kuwa na mpango kazi utakaoweza kuwaongoza vyema katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku na kuweza kupimwa juu ya uwajibikaji wao pasipo shaka.

Anaendelea kufafanua kuwa mpango kazi kwa mtumishi utasaidia kuweza kupata tathimini ya utekelezaji wa majukumu ya mtoa huduma za afya na kujua matokeo yapi yamefanikiwa na kubaini changamoto zilizojitokeza na kuzitafutia suluhisho ili kufikia malengo ya mtoa huduma aliyojiwekea katika mpango kazi wake.

“Ili kupata tathimini ya utendaji kazi wa watoa huduma za afya amesisitiza kuhakikisha kila mmoja kuwa na taarfa ya uwajibikaji wake huku ukiwa na takwimu sahihi wakati wote. Ameongezea Dkt.Gwajima

Aidha Dkt.Gwajima amehitimisha kwa kuwataka watoa huduma za afya kutekeleza mipango kazi yao kwa vitendo ili kuweza kupata matokeo chanya yatakayoonyesha mabadiliko katika sekta ya afya badala ya kuwa na watumishi ambao, ukimuuliza utemdaji kazi wa siku anakuwa  hana maelezo yenye takwimu bayana.

Naye Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dkt.Samwel Seseja amesema kuwa atasimamia vyema maelekezo yalotolewa  ili kuhakikisha utendaji kazi na uboreshaji wa huduma za afya kuanzia ngazi ya msingi hadi Mkoa zinaboreka na kuimarishwa vizuri kwa faida ya watanzania.

Chanzo: Tovuti ya OR-TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz)




Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.