• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Kambi: Watoto wenye mahitaji maalum wanahaki ya kusoma

Imewekwa tarehe: January 12th, 2025

Na. Coletha Charles, CHANG’OMBE

Kata ya Chang’ombe, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imebainisha na kuwaandikisha watoto wenye mahitaji maalum kwa lengo la kujiunga na elimu ya awali na msingi kwa mwaka wa masomo 2025 kwa kushirikiana na wazazi, walezi na walimu.

Akizungumza wakati wa uandikishaji wa watoto hao, Afisa Elimu Maalum Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Mwl. Issa Kambi, alisisitiza kuwa jukumu la kuwapatia watoto hao fursa ya kusoma lipo mikononi mwa wazazi na walezi kwa sababu wanahaki ya kupata elimu kama watoto wengine kwa kuwajengea msingi bora wa maendeleo. 

 Alisema kuwa, serikali imejipanga kuwahudumia watoto wenye mahitaji maluum kwa kuwapokea na kuwapa mahitaji stahiki na kuhakikisha wanapata nafasi bila kujali changamoto zao. “Wazazi ukiwa na mtoto usichoke kumlea, ukiona umechoka basi huyo mtoto amefanikiwa na tusiwakatie tamaa. Watoto wenye umri wa kwenda shule tushirikiane kuwaleta waje waandikishwe kwenye shule zetu, walimu wapo watawahudumia. Niwaombe muwaambie na wengine waliobaki nyumbani kuwa, tunapokea watoto wa aina zote kulingana na mahitaji yao na tunawahudumia” alisisitiza Mwl. Kambi.

 Nae, Afisa Elimu, Kata ya Chang’ombe, Rebecca Haule, alitoa wito kwa wazazi na walezi kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata fursa ya kuandikishwa shule kwa ajili ya kuanza masomo ili waweze kujifunza na kufikia ndoto zao.

Alisema kuwa, kila mzazi mwenye mtoto ambaye ana umri wa kuanza kusoma anapaswa kumuandikisha ili aanze masomo kwa sababu elimu ni haki yake ya msingi na serikali ya awamu ya sita imeweka mazingira bora na rafiki ya kujifunza. “Kama kata tumejitahidi kuhamasisha na wazazi wamejitokeza, tutaendelea kuhamasisha hadi siku ya mwisho na tunawaomba wazazi na walezi watupe ushirikiano. Tunawaomba wasiache kuwapeleka watoto wenye mahitaji maalum shule, kwa sababu elimu ni msingi wa maendeleo ya mtoto na jamii kwa ujumla” alisema Haule.

 Kwa upande wake, Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Chang’ombe, Mwl. Bakari Mtembo, alitoa wito kwa wazazi kutowafungia ndani watoto wenye mahitaji maalum na badala yake kuwapeleka shule kwa sababu wana haki ya kupata elimu kama watoto wengine. 

Alisema kuwa, ubainishaji wa watoto wenye mahitaji maalum ni hatua muhimu katika kuhakikisha elimu jumuishi inatekelezwa kikamilifu na ushirikiano unahitajika ili kuhakikisha watoto hao wanapata msaada wanaohitaji kufikia ndoto zao. “Mwitikio wa wazazi kuwaleta watoto kuandikishwa kwa ajili ya masomo 2025 umekuwa mkubwa, japo wamefika kwa kuchelewa huenda hawakupata taarifa ya uandikishaji mapema kutoka kwa viongozi wao wa mitaa. Lakini pia shule yetu inapokea watoto wenye mahitaji maalum. Hivyo, wazazi wasione aibu kuwaleta watoto shule” alisema Mwl. Mtembo.

 Aidha, mkazi wa Chang’ombe ambaye ni mzazi wa mtoto mwenye mahitaji maalum, Erika Magomba, aliomba serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwasaidia wazazi wenye watoto wenye mahitaji maalum misaada mbalimbali ya mahitaji katika ukuaji wao. “Niwashauri wazazi wenzangu kutowaficha watoto kwa sababu hawa watoto wengine wanavipaji mbalimbali kama kushona na ufundi. Kwahiyo, tujitahidi tuwatoe watoto nje ili watu wawaone waweze kuwasaidia. Ninawashukuru sana watoto wetu wamepata msaada mkubwa wa kwenda shule” alisema Magombe.

Katika harakati za kuhakikisha watoto wenye mahitaji maalum wanapata haki zao za msingi ya kupata elimu, umuhimu wa kubainisha changamoto zao mapema hauwezi kupuuzwa.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.