• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Uzinduzi Kampeni ya Usafi wa Mazingira yaanza kwa mafanikio

Imewekwa tarehe: January 22nd, 2022

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Joseph Mafuru ameridhishwa na muitikio wa wananchi wa kata ya Makole kujitokeza kushiriki zoezi la usafi wa mazingira na kuwataka kujenga tabia ya usafi wa mazingira kwa vizazi vijavyo.

Kauli hiyo aliitoa alipokuwa akiongea na mamia ya wananchi wa kata ya Makole na maeneo ya jirani baada ya kuhitimisha uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira iliyozinduliwa katika ngazi ya halmashauri kwenye kata hiyo.

Mafuru alisema “mimi niwashukuru sana, mmetoka kwa wingi sana, na bahati nzuri kabla sijaja hapa nilikuwa natembelea kwenye mitaa yenu yote ya kwenye kata. Muitikio ni mkubwa sana.

Jamani usafi unaanzia nyumbani na nikisema usafi unaanzia nyumbani simaanishi nje tu, namaanisha ndani, sebuleni, chumbani kwako na maeneo ya ndani. Ile tabia ya usafi tuendelee kuijenga kwetu na kwa watoto wetu na kwa kizazi kinachokuja. Mimi nina miaka minne Dodoma, tabia hii ya usafi Dodoma ipo na ipo juu, lazima tukubaliane kwa kweli. Tulilegalega kidogo kama miezi sita iliyopita. Tumekubaliana kwenye timu ya wataalam na Baraza la Madiwani kuwa turudi kwenye tabia yetu ya awali. Jumamosi tunakutana tunafanya usafi pamoja na tukimaliza tunakaa tunaongea matatizo yetu na namna bora za kuyatatua” alisema Mkurugenzi Mafuru.

Aidha, Mkurugenzi huyo aliwapa salam za Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Jabir Shekimweri alieyetarajiwa kushiriki katika zoezi hilo kabla hajapata majukumu mengine ya kitaifa.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Mazingira na udhibiti wa taka ngumu wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma, Dickson Kimaro alisema kuwa kampeni hiyo imeanzia katika Kata ya Makole na zoezi la usafi linaendelea katika kata zote za halmashauri hiyo.

“Lengo la usafi huu ni kuhakikisha Jiji la Dodoma linakuwa safi na nadhifu. Tunafahamu wote kuwa Dodoma ni makao makuu ya serikali, hivyo, lazima jiji liwe safi. Tunayo kaulimbiu isemayo ‘mita tano usafi wangu, usafi wangu mita tano’ ikilenga kuihamasisha jamii kufanya usafi katika maeneo yao na maeneo yanayowazunguka.” Alisema Kimaro.

Aidha, Kimaro aliwataka wananchi kutii sheria bila shuruti. “Ndugu zangu tufanye usafi katika maeneo yetu, tutii sheria bila shuruti kwa sababu sheria ndogo tuliyonayo katika Jiji la Dodoma inasema mtu asipojitokeza kwenye usafi, mtu asipofanya usafi kwenye eneo lake la makazi, taasisi na biashara, faini yake ni kati ya shilingi 50,000-200,000 au kifungo kisichozidi miezi sita au vyote viwili kwa pamoja” alisema Kimaro.

Wananchi wa Kata ya Makole wakishiriki kwenye uzinduzi wa kampeni ya usafi wa mazingira leo tarehe 22.01.2022.

Wananchi wakipakia taka kwenye gari wakati wa kampeni ya usafi wa mazingira.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.