Na. Mwandishi wetu, Ng’hong’onha
Kata ya Ng’hong’onha mwenyeji wa maadhimisho ya siku 16 za kupinga ukatili wa kijinsia ngazi ya halmashauri yakilenga kutoa elimu na hamasa kwa jamii dhidi ya kupambana na ukatili katika jamii kuelekea miaka 30 ya Beijing.
Katika maadhimisho hayo elimu dhidi ya ukatili wa kijinsia itatolewa pamoja na kufafanua aina za ukatili wa kijinsia, taarifa za vitendo vya ukatili wa kijinsia na kuwajengea uelewa wanafunzi na watoto kuripoti taarifa za ukatili wa kijinsia katika jamii
Maeneo mengine yatakayopewa kipaumbele ni umuhimu wa kuwainua wanawake kiuchumi kama njia moja wapo ya kupambana na ukatili wa kijinsia.
Maadhimisho hayo yanayoongozwa na kaulimbiu isemayo “Kuelekea miaka 30 ya Beijing: Chagua kutokomeza ukatili wa kijinsia” yanapambwa na burudani mbalimbali kama maigizo na ngoma, mgeni rasmi ni Joseph Chotero, Mkurugenzi wa SABUDA Foundation yakifanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Ng’hong’onha
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.