WAZIRI wa Afya, Ummy Mwalimu alisema kwa mujibu wa takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO) zinaonesha kwamba katika kila vizazi hai 160 mtoto mmoja huzaliwa na tatizo la Usonji Tanzania.
Mwalimu alisema haya aliposhiriki Marathon ya kuchangia huduma za Usonji zilizofanyika katika viwanja vya Green Garden-Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
“Lakini takwimu za sasa kwenye vituo vya huduma za afya na shuleni zinaonesha kuwa takribani watoto 2000 tu ndio wanaopatiwa huduma.” alisema Waziri Mwalimu
Aidha, alisema ukilinganisha na hali ya uzazi nchini ambapo jumla ya wanawake milioni 2.4 hujifungua kila mwaka na kwa makadirio ya WHO inaonesha kuwa kila mwaka watoto zaidi ya 15,000 huzaliwa na tatizo la Usonji kwa kiwango tofauti.
Akielezea tatizo la Usonji Mwalimu alisema kuwa Usonji ni tatizo la kibaiolojia ambalo humkumba mtoto akiwa ndani ya tumbo la mama yake na tatizo hilo hujidhihirisha zaidi mtoto anapofikia umri wa miaka mitatu.
Hata hivyo Mwalimu alisema katika kukabiliana na tatizo la idadi ndogo ya walimu, shule chache zenye uwezo wa kuhudumia watoto wenye mahitaji maalum, Serikali imeanzisha mafunzo ya ngazi ya stashahada (diploma) katika Chuo cha Ualimu Patandi Arusha na vyuo vikuu vingine.
Sambamba na hilo, Mwalimu alibainisha kuwa Kwa kutambua ukubwa wa tatizo hilo Wizara ya Afya imeimarisha huduma za Afya ya Akili pamoja na Huduma za Utengamao ili kuweza kuongeza ufanisi kwenye huduma hizo.
Mwisho, Mwalimu alisema Wizara ya Afya inashirikiana na Sekta nyingine muhimu ikiwemo Sekta ya Elimu, Ofisi ya Waziri Mkuu eneo linaloshughulikia watu wenye ulemavu, Wizara inayoshughulikia masuala ya Maendeleo ya Jamii, wanawake na makundi maalum pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kuhakikisha kuwa wanashirikiana ili kuleta tija katika upatikanaji wa huduma hizi
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.