Na. Mussa Richard, DODOMA
Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi wa Divisheni ya Kilimo Mjini, Halmashauri ya Jiji la Dodoma imeibuka kidedea baada ya kushinda penati 6-5 dhidi ya Timu ya Mpira wa Miguu ya Watumishi wa Divisheni ya Uendelezaji Makao Makuu.
Penati hizo zilipigwa baada ya kutoshana nguvu katika muda wa kawaida ndipo ikaamuliwa kupigwa mikwaju ya penati na Kilimo kuibuka wababe. Mchezo huo ulivurumishwa katika Kiwanja cha Jamhuri Dodoma kwenye Bonanza la kuukaribisha Mwaka 2025 lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
Baada ya mchezo kutamatika Nahodha wa Timu ya Kilimo FC, Michael Lukumai alisema “toka mchezo unaanza sisi tulikua bora kuliko wao japo walianza kwa kututangulia mabao yote lakini sisi tukawa bora kuliko wao, ndiyo maana tukafanikiwa kurudisha mabao yote na kwenye mikwaju ya penati tukaibuka kidedea, lakini yote kwa yote watumishi wamepata burudani na imekuwa siku ya kihistoria kwetu sote”.
Nae, Nahodha wa Timu ya Ardhi FC, Godwin Maselo akaelezea sababu zilizofanya wafungwe huku akiwamwagia sifa wachezaji wenzake kwa kiwango bora walichoonesha. “Mchezo ulikua mzuri na sisi kama Ardhi tulicheza vizuri ndiyo maana tulikua tunawatangulia kufunga mabao na wao wanarudisha, tumekuja kupoteza kwa mikwaju ya penati kwasababu penati hazina mwenyewe. Bahati imekuwa kwao wameshinda, nawapongeza na kila mtu kafurahi siyo kwa Timu ya Kilimo tu bali hata watumishi wengine waliohudhuria katika bonanza hili” alisema Maselo.
Bonanza hilo lililoandaliwa na Halmashauri ya Jiji la Dodoma lilikuwa na lengo la kuwakutanisha watumishi wote na kuukaribisha Mwaka 2025 chini ya kaulimbiu isemayo “Halmashauli ya Jiji la Dodoma Ushirikiano na Umoja wetu ndiyo nyenzo ya huduma b
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.