• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Ma DC wajengewa uwezo kusimamia utoaji wa mikopo ya asilimia 10

Imewekwa tarehe: July 27th, 2024

Na. James Mwanamyoto, OR-TAMISEMI

NAIBU Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Sospeter Mtwale amesema Wakuu wa Wilaya wanapatiwa mafunzo na Ofisi ya Rais -TAMISEMI ya kuwajengea uwezo wa kusimamia zoezi la utoaji na urejeshaji wa mikopo ya asilimia 10 inayotolewa na halmashauri za Wilaya kwa akina mama, vijana na wenye ulemavu.

Bw. Mtwale amesema hayo leo katika Ukumbi wa Shule ya Uongozi ya Mwalimu Julius Nyerere Kibaha mkoani Pwani kwa Niaba ya Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI Bw. Adolf Ndunguru wakati akifungua kikao kazi cha Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe. Mohamed Mchengerwa na Wakuu wa Wilaya zote nchini.

Bw. Mtwale amesema, Serikali imeanza kutoa mikopo ya asilimia 10 baada ya hapo awali kusitishwa kutokana na changamoto jilizojitokeza, na kuongeza kuwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI imeshapitia kanuni na kufanya maboresho na ikaona ni vema Wakuu wa Wilaya wakapitishwa katika kanuni hizo ili waweze kushiriki kikamilifu katika usimamizi wa utoaji wa mikopo hiyo.

“Tumeona ni vema nanyi mkapitishwa katika kanuni hizo ili tuwe na uelewa wa pamoja katika kusimamia utoaji wa mikopo hiyo ili mikopo hiyo iwe na tija kwa watakaonufaika na katika taifa kwa ujumla,” Bw. Mtwale amesisitiza.

Sanjari na hilo, Bw. Mtwale amesema Wakuu wa Wilaya watapitishwa katika taarifa ya ukaguzi ya mwaka wa fedha 2022/23 ili wafahamu hoja zilizoibuliwa na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kwani nao ni wasimamizi wa halmashauri zilizopo katika maeneo yao ya utawala.

Ili kuongeza ufanisi katika utekelezaji wa majukumu ya Wakuu wa Wilaya nchini, Bw. Mtwale amesema Ofisi ya Rais - TAMISEMI imemualika mtaalamu wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Garvin Kweka ili kuwapatia elimu ya afya ya akili na ya namna bora ya kuepukana na magonjwa ya afya ya akili.

Akiwasilisha mada kuhusiana na afya ya akili, mtaalamu wa afya ya akili kutoka Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Dkt. Garvin Kweka amewataka Wakuu wa Wilaya kuzingatia mahusiano ya kijamii ili kujenga afya nzuri ya akili itakayowawezesha kutekeleza kikamilifu majukumu yao kwa ufanisi.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.