• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

'Ma-RC, Ma-DC toeni taarifa upungufu wa chakula' - Waziri Mkuu

Imewekwa tarehe: November 14th, 2019

SERIKALI imewaagiza viongozi wa mikoa na wilaya watoe taarifa kama maeneo yao yana upungufu wa chakula na ni kiasi gani kinahitajika.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa amesema leo bungeni mjini Dodoma kuwa, Wizara ya Kilimo ikipata taarifa hizo itaratibu vizuri na kuona namna ya kufikisha chakula kwa wananchi na kuwauzia ili zipatikane fedha za kununua chakula kingine kiwekwe kwenye Hifadhi ya Taifa ya Chakula (NFRA).

Ameyasema hayo wakati akijibu swali la Mbunge wa Chemba (CCM) Juma Nkamia aliyetaka kauli ya Serikali kwa kuwa baadhi ya mikoa ukiwemo wa Dodoma, Manyara na Singida ina tatizo kubwa la chakula na huenda baadhi ya wenyeviti wa kamati za ulinzi na usalama hawatoi taarifa sahihi kwa sababu ya woga.

“Upungufu wa chakula upo kwa baadhi ya wilaya na maeneo mengine na huu ulitokana na tatizo la hali ya hewa, kwamba yapo maeneo msimu uliopita hayakupata mvua ya kutosha. Jambo hili linapotokea kule kwenye ngazi hiyo tunao viongozi…” amesema Waziri Mkuu wakati akijibu maswali ya papo hapo kutoka kwa wabunge wa Bunge la Tanzania.

“Inapotokea kama hali ya hewa imekuwa mbaya Mkuu wa Wilaya akieleza atakuwa anaeleweka kwa sababu pia baada ya kutoa taarifa hiyo timu ya Wizara ya Kilimo itakwenda kuona hali halisi na kuweza kuzungumza na ile mamlaka kuweza kupelekewa chakula kwa bei nafuu” amesema Waziri Mkuu.

Amesema jambo hilo limetolewa ufafanuzi mara nyingi na kwamba, Rais John Magufuli hajazuia kutolewa kwa taarifa za upungufu wa chakula isipokuwa kwenye maeneo yenye hali nzuri ya hewa na kila mmoja ana nafasi ya kulima au kufanya kazi lakini yana upungufu wa chakula.

“Viongozi waliopo kwenye maeneo hayo wanao wajibu wa kusimamia kila mmoja anafanya kazi pamoja na kulima mazao ya chakula na biashara ili waweze kujipatia tija inapofikia kipindi kama hiki kila mmoja anakuwa na akiba yake” amesema.

Ametoa mwito kwa wafanyabiashara watumie fursa ya tofauti za hali ya hewa kwenye maeneo kuuza chakula sehemu zenye upungufu.

Amewataka wakuu wa wilaya na wakuu wa mikoa wakutane na wafanyabiashara wawashawishi wapeleke chakula kwenye maeneo yenye upungufu ili kuongeza vipato vyao.

Chanzo: habarileo.co.tz


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.