• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maafisa Habari tangazeni miradi ya Serikali – Mhe. Bashungwa

Imewekwa tarehe: May 24th, 2021

MAAFISA Habari waja na kauli mbiu “Utoaji wa taarifa kwa umma ni Takwa la Kisheria, Viongozi wa Umma na Maafisa Habari Tuwajibike”

Ni kauli mbiu iliyotolewa katika Mkutano wa 15 wa kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali kinachofanyika Jijini Mbeya kuanzia leo tarehe 24 hadi 28 Mei 2021 katika ukumbi wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST) na kuhudhuriwa na Maafisa Habari 370 wakiwemo Maafisa Habari 20 kutoka Zanzibar.

Mgeni rasmi katika kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali, Mhe. Innocent Bashungwa ambaye ni Waziri wa Habari, Utamaduni na michezo aliwasiri eneo la mkutano na kupokelewa na katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Dkt. Hassani Abbas pamoja na Sektarieti ya TAGCO na kisha kukagua vibanda vya maonesho mbalimbali chuoni hapo ambapo pia alipata maelekezo ya huduma zitolewazo katika eneo hilo.

Bashungwa alisema lengo kuu la kikao kazi cha Maafisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano wa Serikali limejikita katika kutekeleza kauli mbiu ambayo ni utoaji wa taarifa kwa umma ni takwa la kisheria, Viongozi wa umma na Maafisa Habari tuwajibike,” ambapo miongoni mwa mambo ambayo Serikali inasimamia ni pamoja na namna ya utaoaji habari kwa jamii.

Alisema moja ya kazi ya Afisa habari wa Serikali ni pamoja na kutangaza Miradi ya Serikali, kazi zote zilizotekelezwa na Serikali ili kuuhabarisha umma uweze kufahamu jitihada zilizofanywa na zinazoendelea kufanya na Serikali yao.

Amezitaja baadhi ya changamoto zinazokwamisha utendaji kazi wa Maafisa Habari ni kutoshirikishwa kwenye vikao mbalimbali vya Taasisi, kutotengewa bajeti ya Habari na Mawasiliano, kukosa bando la internet, kutokuwa na vifaa au vitendea kazi vyenye ubora.

Amewataka Waajiri wote nchini kutenga bajeti ya ununuzi wa vifaa bora vya Afisa Habari kama Kompyuta, Kamera, vinasa sauti na kadharika ili aweze kufanya kazi kwa kiwango kinachostahili ikiwemo upatikanaji wa picha nzuri za miradi ya Serikali zenye kiwango pamoja na kutengewa vifurushi vya intaneti kwani Afisa Habari mara nyingi huendelea kufanya kazi wakati wowote hata nje ya ofisi na baada ya masaa ya kazi. Mhe. Bashungwa alisisitiza.

Ametoa wito kwa viongozi wote kuhakikisha wanatatua changamoto zote zinazokikabili kitengo cha Habari na Mawasiliano ili kuwezesha jamii kupata habari sahihi, kwa wakati sahihi na zenye tija kwa jamii na Serikali.

Aidha, pamoja na uwepo wa changamoto za ukosefu wa vitendea kazi amewataka Maafisa Habari hao kuendelea kufanya kazi kwa kujituma kwani anatambua uwepo wa baadhi ya Maafisa Habari ambao hawajitumi kufanya kazi kwenye maeneo yao kwa kigezo hawana vitendea kazi.

Ameshauri wasimamizi wa mfumo wa eGA kwa kipindi kijacho kufuatilia Maafisa Habari ambao wanafanya kazi vizuri kwenye tovuti zao wachukuliwe majina yao ili waweze kupata zawadi ya kufanya kazi vizuri na zenye tija kwa jamii na serikali.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Juma Homera amewataka maafisa habari wote kuwa makini katika kusikiliza maelekezo yanayotolewa na wawezeshaji hao ili yaweze kuwasaidia katika kuboresha utendaji wa kazi na kutangaza miradi yote ya Serikali.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.