• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maafisa Madini Wakazi Mikoa watakiwa kuimarisha mahusiano wao, viongozi wa Serikali

Imewekwa tarehe: September 10th, 2021

Waziri wa Madini, Doto Biteko (pichani juu), amewataka Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa yote ya kimadini nchini kuimarisha mahusiano baina yao na viongozi wengine wa Serikali waliopo katika maeneo yao ikiwa ni pamoja na wakuu wa mikoa, wilaya, watendaji wa kata na viongozi wa vijiji wanakohudumia.

Amesema wao ndio sura ya wizara katika mikoa na wilaya wanazozisimamia na kuwataka kuweka historia nzuri kwenye maeneo yao. “Likitokea jambo baya lolote sote tunachafuka hivyo tuwe makini katika kujenga taswira njema ya sekta yetu” Biteko amesisitiza.

Amesema hayo alipokuwa akifungua Mkutano wa robo ya kwanza ya Mwaka wa Fedha 2021/2022 ambao upo katika Almanac ya Tume ya Madini ya Mwaka 2021/2022 wenye lengo la kujadili juu ya uboreshaji wa mikakati mbalimbali ya namna ya kufikia na hata kulivuka lengo la kukusanya Shilingi 650,000,000,000 walilopangiwa na Serikali kwa mwaka huu wa fedha.

“Suala hili ni jema, na Wizara ya Madini inawaunga mkono na kama ilivyo ada itaendelea kuunga mkono juhudi hizi ambazo zina tija kwa Sekta ya Madini katika kuhakikisha Sekta inafikia mchango wa asilimia 10 kwenye Pato la Taifa ifikapo 2025” ameongeza Biteko.

Amesema kiu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ni kuifanya Sekta ya Madini inaendelea kuwa kinara kwa ukuaji wa uchumi wa nchi na kubainisha kikao hicho ni muhimu kwani kimewahusisha wataalamu wanaosimamia kwa ukaribu zoezi la ukusanyaji wa maduhuli ya serikali.

Aidha, Waziri Biteko amewataka watendaji hao kutumia mkutano huo kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kutokana na mazingira tofauti tofauti waliyotoka, pia kuchangia kwa uhuru na uwazi ili kutoa nafasi kwa viongozi kuona namna bora ya kushirikiana nao katika kutatua changamoto watakazoziibua.

“Wizara imepewa lengo la kukusanya Shilingi bilioni 650,000,000,000 ni kubwa lakini msivunjike moyo kaendeleeni kufanya kazi ili kuifanya Sekta ya Madini iendelee kuwa kinara katika kuchagiza ukuaji wa uchumi wa nchi,” amesema Waziri Biteko.

Pamoja na hayo Waziri Biteko, amewapongeza Maafisa hao kwa namna wanavyofanya kazi katika maeneo yao na kueleza kunapokuwa na hoja inayomlazimu kupata ufafanuzi kutoka kwao asilimia 90 ya Maafisa hao wanakuwa wanaufahamu wa suala husika na wamelifanyia kazi.

Aidha, amewataka Maafisa hao kusimamia haki na kujitenga na mambo ya kuchukua rushwa kutoka kwa wachimbaji kwani litawaharibia sifa kama viongozi walioaminiwa.

“Toa ushauri wako kwa viongozi wako wa Mkoa na Serikali ili kupeana mawazo namna ya kutatua changamoto mnazokutana nazo, "isifike mahali ukaona Sekta ya Madini ni yako, kuna viongozi wengine huko shirikiana nao” amesisitiza Biteko.

Akieleza suala la leseni zinazotajwa kufuta, Waziri Biteko amewataka kufuta leseni mara baada ya kujiridhisha kuwa kweli leseni inasifa ya kufutwa na sio kwa kufuata majungu ya watu na kutaka haki itendeke.

Pia, Waziri Biteko ameelekeza kuwa maeneo yote yenye mfumuko wa Madini (rush) ambayo kuna uwezekano wa kutoa leseni, leseni zitolewe kwa mujibu wa Sheria ili kurahisisha usimamizi.

“Wasaidieni watanzania kufurahia uwepo wa Sekta ya Madini, wahudumie kwa upendo na endeleeni kufanya kazi kwa haki, kwa uaminifu na kila mmoja atende haki, alisisitiza Waziri Biteko”.

Akizungumza kabla ya kumkaribisha waziri Biteko, Naibu Waziri wa Madini, Prof. Shukrani Manya amewapongeza Maafisa hao kwa kazi kubwa wanayoifanya ukilinganisha na ukubwa wa eneo wanalolisimamia na idadi ya watumishi walionao.

Amewataka kuifanyia kazi imani waliyopewa na Serikali kwa kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kikamilifu na kuifanya sifa njema ya Tume ya Madini tangu kuanzishwa kwake inaendelea kuwepo. “Kupitia nyie Wizara ya Madini inaendelea kutengeneza jina jema na tuendelee hivyo” alimaliza Prof. Manya.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula amewataka maafisa hao kuimarisha utendaji kazi wa taasisi na kuwa na mtazamo wa pamoja wa namna ya kuhakikisha wanashirikiana kuimarisha utendaji wao.

Amesema suala la kuhakikisha maduhuli ya serikali yanakusanywa si suala la mzaha na kuhimiza wasimamie kikamilifu suala hilo. “Kama hatuwezi kufikisha malengo hatufai kila mmoja atumie nguvu katika kuhakikisha anafikia malengo aliyowekewa na ikiwezekana kuvuka lengo ulilowekewa”.

Mkutano huu ni wa siku moja unaofanyika katika ukumbi wa Mruma uliopo katika jengo la Taasisi ya Jiolojia na Utafiti Tanzania (GST).

Mwenyekiti wa Tume ya Madini, Prof. Idris Kikula akizungumza jambo katika ufunguzi wa mkutano wa Maafisa Madini Wakazi wa Mikoa uliofanyika Septemba 10, 2021 jijini Dodoma.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.