• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maafisa Mazingira waagizwa kusimamia "Soma na Mti"

Imewekwa tarehe: January 21st, 2022

WAZIRI wa Nchi,Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira,Seleman Jafo amewaagiza Maafisa Mazingira nchini kusimamia kampeni ya ‘soma na mti’ ambayo lengo lake ni  wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo kupanda  miti zaidi ya milioni 14 ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

Pia amesema ukosefu wa mvua katika siku za hivi karibuni umesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kuna wajibu wa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko hayo.

Akizungumza leo Januari 20,2021,Jijini Dodoma  wakati wa uzinduzi wa kampeni ya  upandaji miti kwa wanafunzi wa shule  na Vyuo nchini iitwayo soma na mti,Waziri Jafo amewaagiza Maafisa Mazingira hao kuisimamia kwa vitendo kampeni hiyo lengo likiwa ni kuhakikisha miti mingi inapandwa nchini.

Waziri Jafo amesema ilani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) inazitaka kila Halmashauri kuhakikisha inapanda miti milioni 1.5 lengo likiwa ni kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchini hivyo kwa upande wa kampeni ya upandaji miti kupitia wanafunzi wa shule za msingi,sekondari na vyuo wamepanga kupanda miti zaidi ya milioni 14.

Amesema lengo ni mwanafunzi ajifunie kwamba yeye amepanda pamoja na kuutunza mti kwa ajili ya utunzaji wa mazingira katika shule na vyuo.

Katika hatua nyingine,Waziri Jafo amesema  ukosefu wa mvua katika siku za hivi karibuni umesababishwa na mabadiliko ya tabia nchi hivyo kuna wajibu wa kupanda miti ili kukabiliana na mabadiliko hayo. 

“Mvua ilikuwa inaanza kunyesha kuanzia mwezi wa tisa lakini  leo tuna Januari  lakini mvua haijaanza hii ni kutokana na mabadiliko ya Tabia nchi kiwango cha maji katika mabonde na mito yetu yamepungua pia mgawo wa umeme umerudi kutokana na maji kupungua,”amesema.

Naye,Naibu Waziri Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anaeshughulikia elimu,David Silinde ameagiza kufufuliwa kwa  Klabu za utunzaji  wa mazingira katika shule pamoja na Maafisa elimu kuisimamia kwa vitendo  kampeni ya soma na mti kuhakikisha inatekelezwa kikamilifu.

“Naziagiza shule zote nchini kuanzisha na kufufua Klabu za mazingira hili ni takwa na wala sio ombi nitahakikisha hili tunalitekeleza,”amesema

Kwa upande wake,Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais,Muungano na Mazingira Khamis Hamza Chilo amesema lengo la kuzindua kampeni hiyo ni kuhami viumbe hai,kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi pamoja na kufuata matakwa ya sheria hivyo  amewaomba watanzania kutunza mazingira na kwao liwe zoezi endelevu.

Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Antony Mtaka aliwataka wale wenye viwanja vipya kupanda miti mitatu katika viwanja hivyo   ikiwemo wa kivuli na mti mmoja miwili ya matunda huku akidai kwamba agenda ya utunzaji wa mazingira katika Mkoa huo ni endelevu.

Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu (CWT) Deus Seif amesema wapo pamoja na Rais Samia Suluhu Hassan na kwa upande wa walimu kazi inaendelea.

Naye, mwanafunzi wa kidato cha nne kutoka  shule ya sekondari Dodoma,Monica Marwa ameiomba Serikali kuchimba kisima katika shule ya Dodoma Sekondari ili wanafunzi waweze kumwagilia miti ambayo itapandwa huku akimpongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwawekea mazingita wezeshi ya kijifunzia na kusomea.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.