• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maafisa Utumishi majaribuni

Imewekwa tarehe: June 11th, 2021

NAIBU Waziri, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Deogratius Ndejembi amesema Serikali itawachukulia hatua za kinidhamu Maafisa Utumishi wote watakaobainika kuwadanganya Watumishi wa Umma wenye madai ya malimbikizo ya mishahara kuwa wamewasilisha madai yao Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma kwa ajili ya kufanyiwa kazi wakati sio kweli.

Akizungumza na Watumishi wa Halmashauri ya Mji Kondoa na Halmashauri ya Wilaya ya Kondoa leo Wilayani Kondoa, Mhe. Ndejembi amesema kuna baadhi ya Maafisa Utumishi hawatekelezi wajibu wao kikamilifu na kusababisha Ofisi ya Rais Utumishi kutupiwa lawama na Watumishi.

Amewaelekeza Wakurugenzi kuwasimamia Maafisa Utumishi wao ili watekeleze majukumu yao ipasavyo ikiwemo la kushughulikia fomu za madai ya malimbikizo ya watumishi hao ili yafanyiwe kazi kwa haraka kwa lengo la kupunguza malalamiko ya watumishi ambayo yanashusha ari ya kutekeleza majukumu yao kikamifu.

“Madai ya Watumishi yakichelewa kulipwa, mnasingizia fomu ziko UTUMISHI wakati sio kweli, mara nyingi fomu hizi zinakuwa ziko kwenu Wakurugenzi sababu Maafisa Utumishi wenu kujifanya miungu watu,’” Mhe. Ndejembi ameongeza.

Mhe. Ndejembi amesema madai ya Watumishi ni haki yao ya msingi  kwani wanatumia jasho lao kulitumikia taifa, hivyo wanastahili kulipwa na si hisani.

Akizungumzia changamoto ya upandishwaji madaraja kwa watumishi, Mhe. Ndejembi amewaelekeza Maafisa Utumishi nchini kuhakikisha wanatenda haki kwa wanaostahili kupandishwa madaraja kama Mhe. Rais Samia Suhuhu Hassan alivyoelekeza.

“Tujitume kwa bidii tusimuangushe Mhe. Rais ambaye ameonyesha nia thabiti ya kuwajali Watumishi wa Umma katika kulinda maslahi na haki zao za msingi,” Mhe. Ndejembi amesisitiza.

Aidha, Mhe Ndejembi amewataka Maafisa Utumishi kuwa makini katika mchakato wa kuwapandisha madaraja watumishi wanaostahili kupanda na kuongeza kuwa Afisa Utumishi yeyote atakayebainika kusababisha mtumishi kutopata haki hiyo atachukuliwa hatua.

Mhe. Ndejembi amewasisitiza Watumishi wa Umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na Miongozo katika Utumishi wa Umma ili kuboresha utendaji kazi utakaowezesha utoaji wa huduma bora kwa umma.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Kondoa, Mhe. Sezaria Makota, amemshukuru Mhe. Ndejembi kwa kufika Wilayani humo na kuzungumza na Watumishi ambapo pia amesisitiza uwajibikaji kwa watumishi hao.

Mhe. Makota amesema hapendezwi kuwepo kwa madai ya malimbikizo ya mishahara na ya upandishwaji vyeo ambayo hayajafanyiwa kazi na Maafisa Utumishi katika Wilaya yake na kuongeza kuwa hatosita kuwachukulia hatua watakaoshindwa kutekeleza maelekezo.

Mhe. Mhe. Ndejembi amefanya ziara ya kikazi Wilayani Kondoa kwa lengo la kuhimiza uwajibikaji kwa Watumishi wa Umma wa Halmashauri ya Mji Kondoa na Halmshauri ya Wilaya ya Kondoa.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.