• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Maafisa utumishi wakumbushwa sheria

Imewekwa tarehe: June 18th, 2021

MAAFISA Utumishi nchini wametakiwa kuzingatia Sheria, Kanuni na Taratibu na Maelekezo halali yanayotolewa na Serikali wanapotoa ushauri kwa Viongozi na wanaposhughulikia masuala ya kiutumishi kwa watumishi walio chini yao kwa kutoa ufafanuzi wa kisheria wa masuala ya Kiutumishi pale yanapohitajika.

Afisa Rasilimali Watu kutoka Tume ya Utumishi wa Umma, Bibi Saada Ibrahim amesema haya leo Wilayani Kisarawe wakati wa kutoa huduma ya kusikiliza, kutoa ufafanuzi na kutatua changamoto za kiutendaji zinazowakabili watumishi wa umma. 

“Baadhi ya Watumishi wa Umma na Wadau wetu waliofika kupatiwa ufafanuzi wamesema kuna umuhimu kwa Maafisa Utumishi kutenga muda sehemu zao za kazi ili kuwaelimisha watumishi masuala ya kiutumishi na suala hili linapaswa kuwa ni endelevu. Kutowaelimisha watumishi wa umma umuhimu wa kufahamu Haki na Wajibu wao, kufahamu vizuri Sheria, Kanuni, Taratibu na Maelekezo halali yanayotolewa na Serikali kunasababisha baadhi ya Watumishi  kushindwa kujua Haki zao na wakati mwingine kufanya makosa” amesema bibi Saada Ibrahim.

Kwa upande wake Bwana Amas Mahagala, Afisa Tawala Mwandamizi kutoka Tume ya Utumishi wa Umma amesema kwa muda ambao Maafisa wa Tume wamekuwepo Kisarawe kutoa huduma kwa wadau inaonyesha baadhi ya Maafisa Utumishi pamoja na kupatiwa nyaraka mbalimbali za Kiutumishi ili wazisome, wazielewe na wawaelimishe watumishi walio chini yao, bado baadhi hawafanyi hivyo. Ni muhimu nyaraka hizo wakazitumia kutoa elimu kwa watumishi kuliko kuzifungia nyaraka hizo kwenye saraka.

“Changamoto nyingi za watumishi zinazotolewa ufafanuzi hapa zingeweza kupatiwa ufumbuzi na Maafisa Utumishi katika Ofisi zao. Miongoni mwa masuala tuliyowaelimisha wadau wetu ni kuhusu Sheria ya Utumishi wa Umma sura ya 298 (marejeo ya mwaka 2019), hususan ufafanuzi wa kubadilishwa kada, masuala ya likizo, uhamisho, OPRAS, kupandishwa cheo pamoja na masuala ya nidhamu, rufaa na malalamiko.” Amesema Bwana Mahagala.

Miongoni wa wadau waliofika Kisarawe na kupata ufafanuzi wa masuala ya kiutumishi ni Bwana Abdul Ngatila ambaye alitoa maoni yake kuwa Maafisa Utumishi wanapaswa kutambua umuhimu wa kufanya kazi zao kwa weledi na umakini mkubwa kwa sababu wanahusika na maisha ya watumishi, haki na wajibu wa watumishi. Afisa Utumishi asipokuwa makini katika kushughulikia suala la mtumishi husababisha malalamiko pale mtumishi akibaini kuwa hakutendewa haki. Bwana Ngatila alitoa ari kwa Maafisa Utumishi kutimiza wajibu wao huku suala la utunzaji wa kumbukumbu wafahamu nalo kuwa ni jambo la msingi.

Tume ya Utumishi wa Umma, itahitimisha siku ya utoaji huduma kwa watumishi na wadau wake katika Wilaya ya Kisarawe kesho Ijumaa tarehe 18 Juni, 2021 na kuanzia Jumatatu tarehe 21-23 Juni, 2021 Maafisa wa Tume watakutana na wadau katika Ofisi ya Tume iliyopo Mtaa wa Luthuli, Jijini Dar es Salaam.

Imetolewa na:

Kitengo cha Mawasiliano Serikalini

Tume ya Utumishi wa Umma.

KISARAWE- PWANI

17 Juni, 2021

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.