• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mabula ataka kasi zaidi ardhi Dodoma

Imewekwa tarehe: September 30th, 2021

Na Hassan Mabuye, Dodoma

NAIBU Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. Dkt. Angeline Mabula amewataka watumishi wa sekta ya ardhi wa mkoa wa Dodoma kuongeza kasi ya uandaaji na utoaji hatimiliki za ardhi kwa wananchi.

Dkt. Mabula ametoa agizo hilo mwanzoni mwa wiki hii wakati alipokutana na viongozi pamoja na watendaji wa sekta ya ardhi katika halmashauri za wilaya ya Kondoa, Chemba, Bahi na Chamwino katika ziara yake ya kukagua maendeleo ya sekta ya ardhi katika wilaya hizo za mkoa wa Dodoma.

Ameelekeza, kila ofisi ya halmashauri katika mkoa wa Dodoma kuandaa na kutoa angalau hatimiliki za ardhi 100 kila mwezi kwa kuwa kuna baadhi ya halmashauri ambazo amezitembelea na amekuta zinatoa zaidi ya hatimiliki za ardhi 300 katika kila mwezi.

“Huwezi kuwa na lengo la kuandaa hati 120 kwa mwaka, haiwezekani hata kama kungekuwa na mtumishi mmoja, haiwezekani. Nendeni mkapitie upya malengo yenu, labda mgeniambia haya ni malengo ya miezi mitatu sawa lakini sio malengo ya mwaka mzima”

Naibu Waziri Mabula alitoa muda wa hadi kufikia tarehe 21 Oktoba 2021 halmashauri hizo zijipange kuanza kutoa elimu kwa wananchi kuhusu faida za umiliki wa ardhi kwa hati na amemuagiza Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma kufuatilia kwa karibu.

Aidha, Kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Dodoma, Thadei Kabonge amewataka watumishi wa sekta ya ardhi mkoa wa Dodoma kuepuka kuzalisha migogoro mipya hasa ile migogoro ambayo inazalishwa na uzembe wa watumishi wenyewe kwa kuwa inachangia katika kuchelewesha umilikishaji wa ardhi kwa wananchi.

Katika hatua nyingine Afisa Utumishi kutoka Ofisi ya Kamishna wa Ardhi Msaidizi mkoa wa Dodoma, Swaumu Muganyizi amewataka watumishi wa sekta ya ardhi kuwa waadilifu na kuboresha utoaji huduma kwa wananchi na kuepuka rushwa hasa katika umilikishaji.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.