WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali imeunda madawati 1,393 ya ulinzi na usalama wa mtoto katika shule za msingi na sekondari ili kupinga ukatili dhidi ya watoto shuleni na nje ya shule.
Majaliwa amesema madawati hayo yameundwa katika mwaka wa fedha 2022/2023 kwenye mikoa ya Rukwa, Arusha, Tanga, Dar es Saalam, Pwani, Shinyanga, Dodoma nanGeita.
Vilevile, Waziri Mkuu amesema mabaraza 560 ya watoto yameundwa kwa lengo la kutoa fursa kwa watoto kutoa maoni yao kwa uhuru na kuwajengea uwezo wa kujiamini, kujieleza na kujifunza masuala mbalimbali yanayohusu haki na ustawi wao.
Ameyasema hayo wakati akiwasilisha hotuba kuhusu Mapitio na Mwelekeo wa Kazi za Serikali na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Ofisi ya Bunge kwa mwaka 2023/2024 bungeni jijini
Dodoma.
Kadhalika, Waziri Mkuu amewasisitiza viongozi wote wa Serikali, dini, kimila na vyama vya siasa kukemea kwa nguvu zote ushiriki wa jamii katika matendo yasioendana na mila, tamaduni na desturi za Watanzania.
"Hii ni pamoja na wazazi na walezi wote kushirikiana na Serikali katika makuzi na malezi bora ya watoto yatakayowaepusha na vitendo viovu. Serikali imeendelea kuhamasisha jamii kushiriki katika ulinzi na usalama wa mtoto ili kutokomeza ukatili dhidi yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.