Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma Profesa Davis Mwamfupe, leo Januari 8, 2018 amewaapisha Madiwani wawili walioshinda katika chaguzi ndogo zilizofanyika mwishoni mwa mwaka 2018 jijini hapa.
Madiwani walioapishwa ni wale waliohapa kutoka vyama pinzani kutokana na kile walichokieleza kuwa ni kuridhishwa na utendaji kazi wa Serikali ya awamu ya tano ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) ikiongozwa na Mheshimiwa Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Mara baada ya kuwaapisha madiwani hao, Profesa Mwamfupe amewataka madiwani hao kufanya kazi kwa bidii na weledi ili kuleta maendeleo katika jiji la Dodoma, huku akisisitiza zaidi suala la mshikamano.
Hata hivyo, kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini Mhe. Robert Mwinje akizungumza mara baada ya kushuhudia kiapo hicho, mbali na kutoa pongezi, amesema kuwa hatosita kuwachukulia hatua viongozi watakaobainikia kukichafua chama hicho na kuleta mipasuko.
Madiwani walioapishwa ni pamoja na Diwani wa Kata ya Makulu Mheshimiwa Paschal Matulawa pamoja na Mheshimiwa Samweli Mziba wa Kata ya Hazina.
Mheshimiwa Paschal Matulawa akila kiapo cha utii mbele ya Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma
(hayupo pichani) katika ofisi kuu ya jiji
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.