Na. Faraja Mbise, DODOMA
Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, wametakiwa kuwa na uthubutu katika kufanya maamuzi ya kimaendeleo ili kuwanufaisha wananchi wanaowasimamia. Hayo yalisemwa na Mstahiki Meya wa Jiji la Dodoma, Prof. Davis Mwamfupe, alipokuwa akiwakaribisha madiwani kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kyerwa, mkoani Kagera, katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya Jiji la Dodoma.
“Kikubwa katika mtakachokiona, sio utajiri wetu wa pesa ni uthubutu wa kufanya maamuzi, unaweza kuwa na pesa lakini hauna uthubutu wa kuzitumia, ukipewa shilingi milioni moja, utapata wasiwasi kuzitumia kwasababu zitaisha, hutakubali matumizi ya laki mbili au tatu. Lakini sisi hatuogopi, kama tuna mradi wa hoteli iliyopo hapa ambayo imegharimu shilingi Bilioni 12, hatuogopi mradi wa Soko la wazi la Machinga, ingawa serikali ilituchangia shilingi Bilioni tatu, na sisi tukaweka shilingi bilioni sita nyingine. Hatuogopi kwamba tuliwekeza katika mradi na hoteli na ukumbi kule Mtumba, ambao kwa awamu mbili tulipanga uwe na shilingi bilioni 54. Karibuni Dodoma muweze kuangalia matokeo ya uthubutu wetu wa kufanya maamuzi. Sisi hatupendi kujadiliwa kwanini hatukuamua tunapenda tushtakiwe kwanini mliamua vibaya” alisema Prof. Mwamfupe.
Akizungumzia suala la maendeleo, aliwataka waheshimiwa madiwani kuunga mkono juhudi za Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika kukuza uchumi wa nchi na kutoa rai kuwa, wananchi wahudumiwe vizuri bila kutengeneza kero. “Tuungane na Mheshimiwa Rais, kuhakikisha kwamba, tunafikisha maendeleo bila kero yoyote kwa wananchi wanaotegemea huduma yetu” alisisitiza Prof. Mwamfupe.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.