• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

MAGEUZI YA ELIMU TANZANIA YAVUTIA NCHI NYINGINE KUJIFUNZA

Imewekwa tarehe: July 7th, 2025

Mageuzi makubwa yaliyofanyika katika sekta ya elimu nchini, hususan mafunzo ya Amali yameanza kuvutia mataifa mengine barani Afrika kuja kujifunza namna yalivyofanyika na utekelezaji wake.

Hayo yalibainishwa jijini Dodoma kufuatia ziara ya Waziri wa Elimu ya Juu, Utafiti, Sayansi na Teknolojia kutoka Jamhuri ya Gambia, Prof. Pierre Gomez ambaye alisema kuwa lengo la kufika Tanzania ni kujifunza mbinu zilizotumika katika kufanya maboresho na maugezi makubwa katika sekta ya elimu. 

Waziri huyo alisema kuwa Benki ya Dunia iliishauri nchi hiyo kuja Tanzania ili kujionea namna utekelezaji wa Sera, mikakati na miradi mbalimbali katika sekta ya elimu ili kuwawezesha kutekeleza miradi yao kwa ufanisi na tija.

“Tumeshuhudia ujenzi wa miundombinu na mifumo ya mafunzo ya vitendo yenye tija katika vyuo mbalimbali ikiwemo DIT, VETA na Taasisi, tunaamini kunufaika zaidi kupitia ushikiano katika nyanja mbalimbali za mafunzo” alisema Prof. Gomez.

Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia wa Tanzania Prof. Adolf Mkenda amesema Tanzania iko tayari kushirikiana na Gambia katika kubadilishana wakufunzi na wanafunzi ili kuimarisha uhusiano wa kielimu kati ya nchi hizo mbili.

“Tunaamini kuwa kwa kushirikiana, tutaweza kuinua viwango vya elimu ya amali barani Afrika na kusaidia vijana kupata ujuzi unaohitajika katika soko la ajira,” alisema Prof. Mkenda.

Ziara hiyo ni ushahidi wa namna mageuzi ya elimu nchini yanavyotambuliwa kimataifa, na jinsi ambavyo nchi inavyojenga nafasi yake kama kitovu cha ubunifu na ubora katika elimu ya amali Afrika.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Shekimweri: Maafisa tarafa na Watendaji wa kata zingatieni Maadili na Uwajibikaji

    July 23, 2025
  • Serikali yatoa bilioni 298 kugharamia matibabu ya Kifua kikuu, Ukimwi na Malaria nchini

    July 22, 2025
  • Ushirikiano kati ya tanzania na canada waipaisha sekta ya afya

    July 21, 2025
  • Vifaa vya kupima maji vitumike mara baada ya mafunzo

    July 20, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.