• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Majaliwa aagiza wadau kuimarisha ushirikiano kuokoa mazingira

Imewekwa tarehe: June 5th, 2022

Na Mwandishi Wetu, Dodoma

Waziri Mkuu, Kasim Majaliwa amesema kuwa kutokana na kuongezeka kwa uharibifu wa Mazingira, aagiza Wizara na Taasisi husika, pamoja na wananchi kwa ujumla, kuimarisha ushirikiano katika kukomesha uvamizi na uharibifu wa mapori tengefu kote nchini.

Waziri Majaliwa, ameyasema hayo leo Jijini Dodoma katika kilele cha maadhimisho ya siku ya Mazingira Duniani yanayoadhimishwa Juni 5 ya kila mwaka yakienda sambamba na kaulimbiu isemayo "Tanzania Moja tu, Tunza Mazingira" amesema Majaliwa.

"Halmashauri za Miji, Serikali za vijiji na mitaa kote nchini wekeni mikakati ya kukomesha uchomaji moto ovyo. Nawasihi tutoe ushirikiano wa kutosha katika kuhakikisha tunarejesha misitu, ikolojia na uoto wa asili katika maeneo yenu, hususan maeneo ambayo miti ya asili iko kwenye tishio la kutoweka" alisema.

Aidha, amesema kutokana na mwenendo wa hali ya mazingira nchini ipo haja ya kuimarisha mipango na mikakati ya utekelezaji wa uhifadhi na usimamizi wa mazingira ambayo ni vema ikawa shirikishi ikijumuisha ufuatiliaji, usimamizi thabiti na kufanya tathmini ya mara kwa mara ya hali ya mazingira nchini.

"Uhifadhi wa mazingira ni suala endelevu, linalopaswa kuwa shirikishi na kufanywa kila siku. Hivyo, basi, ni matarajio yangu kuwa, wakati wote shughuli za uhifadhi na usimamizi wa mazingira zitaendelea kuwa sehemu ya maisha yetu ya kila siku." amesisitiza Majaliwa.

Katika hatua nyingine, Waziri Majaliwa ameitaka Wizara ya Fedha na Mipango kuhakikisha Mpango Kabambe wa Usimamizi na Hifadhi ya Mazingira unakuwa sehemu ya vipaumbele vya bajeti vya kila mwaka kwa kipindi chote cha utekelezaji wake wa miaka kumi (10).

"Wizara za kisekta, Mamlaka za Serikali za Mitaa zihakikishe Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira unajumuhishwa katika mipango na Bajeti zao, sambamba na kufanya ufuatiliaji wa mara kwa mara na kuwasilisha taarifa ya utekelezaji Ofisi ya Makamu wa Rais" ameongeza Majaliwa.

Naye, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano na Mazingira, Dkt. Seleman Jafo amesema wameendelea kusimamia na kutaratibu ajenda ya mazingira ili kuhakikisha nchi inafanya vizuri katika utunzaji wa Mazingira.

"Nchi imeendelea kupanda miti ikienda sambamba na program ya mazingira. Tunatekeleza ajenda ya upandaji miti Kwa lengo la kuilinda Tanzania. Tuyatunze Mazingira, jukumu letu ni kuhakikisha kazi ya Mazingira inakwenda mbele" amesema Dkt. Jafo.

Kwa upande wa Mratibu Mkazi wa Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, Bw. Zlatan Milisic, amesema familia ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali na wadau wengine kuunga mkono jitihada zinazohimiza utunzaji wa mazingira na teknolojia endelevu ambazo ni rafiki zaidi kwa mazingira.

"Tutaendelea pia kuiunga mkono Serikali katika utekelezaji, ufuatiliaji na tathmini ya mipango mikakati, sera na mikakati ya kitaifa ya mazingira na tabianchi." amesema Zlatan.

Hatahivyo, katika Maadhimisho hayo umezinduliwa Mpango Kabambe wa Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira pamoja na kutoa tuzo kwa Mabalozi wa Mazingira.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.