WAZIRI Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa (Mb) amempongeza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi na kumtaka kuendelea kufanya ubunifu wa kuliboresha jiji la Dodoma ili liwe Jiji la mfano Tanzania na kimataifa.
"Mkurugenzi nimeona jitihada zako ni nzuri na plani zako ni nzuri, kuelekea mpaka Bahi huko kuwe na eneo jingine ili ivute watu wengi zaidi kujenga, simamia ujenzi wa kimkakati kama ulivyosema, eneo hili linahitaji maghorofa na nyumba za kawaida basi angalau rangi zako za bati simamia ili iwe na sura ya kuvutia" alisema Waziri Mkuu.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi amesema bado wana kazi kubwa ya kupokea makao makuu na kujenga jiji kimkakati zikiwemo barabara, soko, stendi, maegesho ya magari na maeneo mbalimbali ya burudani.
Jumla ya shilingi bilioni 77.8 zinatumika kujenga miradi mbalimbali kwa usimamizi wa Jiji la Dodoma kupitia mradi wa Uendelezaji Miji ya Kimkakati Tanzania (TSCP).
Aidha, Waziri Mkuu Majaliwa amemwagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kutenga fedha za kuzungusha kuta katika maeneo yote ya makaburi katikati ya Jiji la Dodoma.
Tembelea Facebook: Dodoma Jiji, Twitter: @DodomaJiji, Youtube: Dodoma City TV
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.