• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Majaliwa: Rais Samia amedhamiria kuendeleza michezo nchini

Imewekwa tarehe: October 22nd, 2021

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Rais wa awamu ya sita Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan anapenda na kuthamini michezo mbalimbali nchini na atahakikisha inaendelea kushamiri na kuongeza tija.

Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wadau wa michezo na wanamichezo wote nchini kwamba Serikali itaendelea kuunga mkono shughuli zote za michezo ukiwemo mchezo wa mpira wa miguu.

Mheshimiwa Majaliwa aliyasema hayo jana usiku (Alhamisi, Oktoba 21, 2021) katika hafla ya utoaji wa tuzo kwa wanamichezo waliofanya vizuri msimu wa 2020/2021 zilizoandaliwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

“Mheshimiwa Rais Samia anawahakikishia kuwa Serikali anayoiongoza imedhamiria kuendeleza michezo na itaongeza nguvu ili kuhakikisha mchezo wa mpira wa miguu nchini unakuwa na viwango bora.”

Waziri Mkuu aliupongeza uongozi wa TFF kwa kuandaa wa tuzo hizo ambazo zinatoa motisha kwa wachezaji, walimu, viongozi wa vilabu na waamuzi. “Tuzo hizi zinaongeza hamasa kwa wengine kushiriki kikamilifu.”

“…Katika vipindi vyote, sasa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania limetufikisha mahali ambapo tunaona muelekeo wa soka letu. Viongozi wa TFF wametufikisha mahali pazuri, tunapaswa kuwapongeza kwa hatua hii.”

Wakati huo huo, Mheshimiwa Majaliwa alimuagiza Mkurugenzi wa Michezo nchini Yusuph Singo ahakikishe timu zinazoliwakilisha Taifa katika mashindano mbalimbali ya kimataifa zinawezeshwa kushiriki kikamilifu bila ya kukwama.

Katika hafla hiyo, Mheshimiwa Majaliwa alitoa tuzo kwa timu na wachezaji waliofanya vizuri katika makundi mbalimbali.  Baadhi ya tuzo zilizotolewa ni na ya mchezaji bora VPL 2020/ 2021 ambaye ni John Bocco kutoka klabu ya Simba; Mchezaji bora wa Kombe la Shirikisho, Feisal Salum kutoka Yanga Sports Club, mchezaji bora anayechipukia ambayo iliyochukuliwa na Abdul Sopu wa Coastal Union na tuzo ya mhamasishaji bora iliyochukuliwa na Nick Reynolds maarufu kama Bongo Zozo.

Tuzo nyingine ni ya timu yenye nidhamu iliyochukuliwa na Timu ya Coastal Unioan, tuzo ya heshima kwa soka la wanawake iliyopokelewa na Mjane wa marehemu, Dkt. Maneno Tamba.

Rais wa Shirikisho la Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia alimkabidhi Waziri Mkuu tuzo ya heshima kutokana na mchango wake mkubwa katika kuendeleza mpira wa miguu nchini. Pia Waziri Mkuu alimkabidhi Alhaji Abdallah Kibadeni tuzo ya mchezaji gwiji.

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.