MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amezitaka Halmashauri za Mkoa wa Dodoma kutunga Sheria Ndogo zitakazomtaka kila Mkazi wa eneo katika Mkoa huo kupanda miti ili kupambana na mabadiliko ya hali tabia Nchi.
Makamu wa Rais ametoa agizo hilo kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuufanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani iliyofanyika Desemba 21 mwaka huu katika eneo la Mzakwe Kata ya Makutupora Manispaa ya Dodoma.
Alisema upandaji miti si kwa ajili ya kuhifadhi mazingira tu bali ni fursa ya kiuchumi, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi ambapo alitolea mfano mti mmoja uliokomaa unaweza kunyonya kiasi cha kilogramu 150 za gesi ya hewa ya ukaa kwa mwaka na hivyo kusaidia kupunguza joto kwenye uso wa dunia, na pia kusaidia kuboresha afya ya mwili na akili.
“Ni dhahiri, kampeni hii ya kuifanya mji wa Dodoma kuwa wa kijani ni kuunga mkono uamuzi wa Rais wetu, Dkt. John Pombe Magufuli wa kuhamishia Makamo Makuu ya Nchi kutoka Dar es Salaam kuja Dodoma kwa vitendo.” Alisema.
Akihojiwa na Vyombo vya Habari wakati wa zoezi hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma Godwin Kunambi alisema Manispaa ya Dodoma imejipanga kuugeuza Mji wa Dodoma kuwa kivutio kikubwa kimazingira kwani pamoja na kuhakikisha inasimamia na kutekeleza kwa ukamilifu program iliyozinduliwa na Makamu wa Rais, pia Manispaa itatenga eneo maalum la ukanda wa kijani (Green Belt) ili kuufanya Mji huo kuwa wa kipekee nchini.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.