WAZIRI MKUU Mhe. Kassim Majaliwa amewatoa hofu Watanzania kuhusiana na kuwepo kwa makontena yenye makinikia ambayo yameonekana yakisafirishwa kwenda nje ya nchi kuwa makontena yanasafirishwa kihalali.
Waziri Mkuu ameyasema hayo bungeni Jijini Dodoma wakati akijibu maswali ya papo kwa papo kwa Waziri Mkuu kitendo ambaho hufanyika kila siku ya Alhamisi iwapo Waziri Mkuu atakuwepo bungeni.
Amesema makontena hayo yanasafirishwa chini ya utaratibu maalum ambao umewekwa na Serikali kupitia kampuni ya umma ya madini ya Twiga kwa kushirikiana na wachimbaji wakubwa wa madini.
“Makontena yote yanayosafirishwa tayari yameshauzwa Serikali imeshapata fedha yake, na fedha zimeshahifadhiwa kwenye akaunti zetu na Watanzania hatupati hasara.” Amesema Waziri Mkuu Majaliwa.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.