Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Suluhu Hassan, ametembelea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma (General Hospital) na kuwafariji majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea jana Januari 2, 2021 Dodoma.
Akiwa hospitalini hapo Mama Samia ametembelea wodi zote na kuwaona majeruhi ambapo wengi wao wanaendelea vizuri.
Aidha ameeleza hatua ambazo zimechukuliwa mpaka sasa ikiwemo kuwasaidia usafiri wa kuendelea na safari abiria waliotoka salama pamoja na majeruhi wanaopona ili kuweza kurejea makwao salama.
Makamu wa Rais, Mama Samia aliongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge na viongozi wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto.
Makamu wa Rais Mama Samia (wa pili kulia) akiongozana na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Binilith Mahenge (wa kwanza kulia) walipotembelea majeruhi wa ajali ya treni iliyotokea Bahi mkoani Dodoma.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.