• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mameya, Wenyeviti Halmashauri wampongeza Rais Samia kuibadili Dodoma

Imewekwa tarehe: June 29th, 2022

MAMEYA na Wenyeviti wa Halmashauri zote nchini wamempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwenye Mamlaka za Serikali za mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo nchini.

Pongezi hizo zimetolewa leo tarehe 29 Juni, 2022, baada ya viongozi hao kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali katika Jiji la Dodoma. Miradi ambayo imetembelewa ni ule wa ujenzi wa jengo la Ikulu ya Chamwino, ujenzi wa Mji wa Serikali ' Magufuli City' na ujenzi wa jengo la Machinga.

Akizungumza kwa niaba ya Mameya na Wenyeviti wa Halmashauri, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ubungo, Mhe Japhari Juma Nyaigesha amesema  Rais Samia  anapaswa kupongezwa na kushukuru kwa kuwaletea wananchi miradi ya maendeleo.

Aidha, ametumia fursa hiyo kuahidi kuhakikisha wanasimamia kwa weledi na umakini miradi inayoletwa na Serikali katika Halmashauri zao ili wananchi waweze kunufaika na miradi hiyo. "Serikali imekuwa ikipeleka fedha nyingi kwenye Halmashauri kwa lengo la kuhakikisha miradi inatekelezwa na kukamilika kwa wakati, hivyo ni jukumu letu kuhakikisha fedha zinazotolewa zinatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan amekuwa akipeleka fedha nyingi kwenye halmashauri, hivyo ni wajibu wetu wastahiki mameya na wenyeviti wa halmashauri kuhakikisha tunasimamia kwa umakini mkubwa ili kumsaidia Rais aweze kutimiza majukumu yake ya kuwahudumia wananchi.”

Naye Mkurugenzi wa Sera na Uratibu, Ofisi ya Waziri Mkuu Paul Sangawe amewataka viongozi hao kuwa na maono na dira kwa kutafsiri kwa vitendo ambavyo wananchi wataweza kuona na kuhakikisha wanasimamia mipango ya maendeleo kwa kutumia mapato ya ndani ili kuleta maendeleo kwa wananchi.

Pia amewataka  kuhakikisha wanaunga mkono juhudi za viongozi wa kitaifa kwa kuhakikisha wanawaeleza wananchi kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na Serikali  kwenye maeneo yao.

Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Chemba, Comrade Sambala Saidi  amesema wao kama  viongozi wana wajibu wa  kudumisha ushirikiano baina ya Mameya, wenyeviti wa Halmashauri na Manejimenti za Halmashauri ili kuhakikisha wanaleta maendeleo  kwa jamii na kuhakikisha miradi inakamilika kwa  wakati.

Kwa upande wa Katibu wa kikosi kazi cha Taifa cha kuratibu Serikali kuhamia Dodoma na ujenzi wa Mji wa Serikali, Meshack Bandawe  amesema ujenzi wa awamu ya pili wa majengo katika Mji wa Serikali unaendelea vizuri na kuwa mkakati ni kuwa ifikapo Oktoba 2023  majengo hayo yatakuwa yamekamilika.

Chanzo: Tovuti ya OR-TAMISEMI 


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.