• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mamlaka Serikali za Mitaa zaagizwa

Imewekwa tarehe: November 20th, 2020

KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga amewaagiza viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanatoa elimu kwa watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla kuhusu uwepo Kituo cha kutolea huduma kwa wateja kilichoanzishwa na Ofisi ya Rais- TAMISEMI.

Akiongea kwenye ziara iliyofanywa na waandishi wa habari katika Kituo hicho leo Mhandisi Nyamhanga amesema lengo la kuanzishwa kwake ni kuwaondolea adha watumishi wa umma na wananchi kwa ujumla kusafiri mpaka Makao Makuu Ofisi za Rais TAMISEMI kwa ajili ya kupata huduma

Amesema Ofisi ya Rais TAMISEMI inahudumia wateja mbalimbali ikizingatiwa kuwa ndio wasimamizi wa Mikoa 26, Wilaya139, Halmashauri 185, tarafa 570, kata 3956, vijiji 12,319, Mitaa 4,263, vitongoji 12,384 na zaidi ya watumishi asilimia 73 ya wanatoka katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, hivyo ni vyema kituo cha kutolea huduma kwa wateja kilichoanzishwa kikatangazwa kuanzia ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa

Amefafanua kuwa kujulikana kwa kituo hicho kutasaidia kupunguza mlundikano wa Watumishi wa Umma na wananchi kwa ujumla kusafiri umbali mrefu na kuja katika Ofisi ya Makao Makuu kufuata huhuma mbalimbali.

“Wateja wakiwemo watumishi wamekuwa wakisafiri umbali mrefu kuja kupata huduma Makao Makuu, Jambo ambalo lilikuwa likileta usumbufu mkubwa, lakini tangu kuanzishwa kwa kituo hiki kumesaidia kupunguza mlundikano wa wateja na kupunguza gharama kubwa, muda na usumbufu kwa wanananchi ambao walikuwa wanakuja kufuatilia masuala mbalimbali” Amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Ametoa wito kwa wananchi wote wanaohitaji kupata huduma mbalimbali katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kukitumia kituo cha kutolea huma kwa wateja ili kuweza kupata huduma stahiki na haraka na amewaagiza watumishi wote kuhakikisha wanakitangaza ili wananchi wakijue na kukitumia.

Akitoa taarifa ya mafanikio Msimamizi wa Kituo Bi. Antelma Mtemahanji amesema mpaka sasa wameweza kupokea simu 15,886, ambapo wateja waliosajiliwa ni 5571 na hoja zilizokamilika na kufungwa ni 5526 sawa na asilimia 99

Mtemahanji anafafanua kuwa kablaa ya kuanzisha kituo hicho Ofisi ya Rais TAMISEMI ilikuwa ikipokea takribani wageni 87 hadi 129 kwa siku lakini kwa sasa inapokea wageni kati ya 20 hadi 47 kwa siku kwa ajili ya kupata huduma mbalimbali.

Amesema kuwa katika kipindi cha miezi mitatu tangu kituo kuanza wateja zaidi ya 5571 wangefika Makao makuu kutoka maeneo mbalimbali ya nchi kufuata huduma hivyo kuanzishwa kwa kituo hiki kimesaidia kupunguza msongamano katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI

Ametoa wito kwa wananchi na watumishi wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kukitumia kituo hiki ili kupata hudum kwa haraka na wakati

Aidha waandishi wa Habari mkoani Dodoma walifanya ziara ya siku moja katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa lengo la kufahamu mafanikio yaliyopatikana tangu kuanzishwa kwa kituo cha kutolea huduma kwa wateja Agosti 6, mwaka huu.


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.