• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Mashindano ya Taifa ya Afya na Usafi wa Mazingira yazinduliwa Jijini Dodoma

Imewekwa tarehe: June 12th, 2019

Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imezindua mashindano ya taifa ya afya na usafi wa mazingira yatakayoratibiwa nchi nzima.

Akizungumza mbele ya waandishi wa habari katika ukumbi wa bunge jijini Dodoma, Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Faustine Ndugulile amesema lengo la mashindano hayo ni kuinua hali ya afya na usafi wa mazingira katika ngazi ya kaya na taasisi ili kulinda na kuboresha afya ya jamii.

“Mashindano haya yalianza mwaka 1988 ambapo yamekuwa yakifanyika kila mwaka. Kupitia mashindano haya hali ya usafi wa mazingira imeendelea kuimarika mwaka hadi mwaka na kusaidia kupunguza magonjwa ya kuhara kutoka zaidi ya wagonjwa 1,300,000 mwaka 2014 hadi chini ya wagonjwa 70,000 mwaka 2018”. Amesema Dkt. Ndugulile.

Aidha, Naibu Waziri huyo amesema mashindano hayo yamesaidia ujenzi wa madampo ya kisasa katika mikoa ya Dodoma, Mbeya, Arusha, Kigoma na Mtwara. Pia ujenzi wa machinjio ya kisasa katika miji mbalimbali  umeweza kutekelezwa na mashindano.

Dkt. Ndugulile ameongeza kuwa mashindano hayo kwa mwaka 2019 yatahusisha Halmashauri zote 184 ambapo Halmashauri zitakazoshinda ngazi ya mkoa zitashindanishwa kitaifa, pia vipengele viwili vimeongezwa katika mashindano ya mwaka huu.

“Ili kuongeza chachu katika mashindano haya, Wizara imeongeza vipengele viwili ambavyo ni ofisi za Makatibu Tawala wa Mikoa na Taasisi za kibenki. Katika Mkoa Benki itakayoshinda itashindanishwa na mikoa mingine ili kupata mshindi wa kitaifa”. Amesema Dkt. Ndugulile.

Mashindano hayo yataendeshwa na kamati ya taifa ya mashindano ya usafi wa mazingira inayojumuisha wajumbe kutoka wizara na taasisi mbalimbali na pia yatakua  na muundo wa makundi 12 ambapo kila kundi litatoa washindi watatu. Makundi hayo ni Halmashauri za majiji na manispaa, Halmashauri za Miji, Halmashauri za Wilaya, Kijiji bora kinachotekeleza kampeni ya usafi wa mazingira, Hospitali za Rufaa za Mikoa, Hospitali za Rufaa za binafsi, Hoteli, Shule za sekondari na msingi, Shule za serikali za sekondari za bweni, Shule za binafsi za sekondari za bweni, Ofisi za umma na Mabenki.

Dkt. Ndugulile amesema Wizara imepanga kutoa zawadi mbalimbali kwa washindi wa makundi ambapo watapatiwa fedha taslimu, vyeti na vikombe. Mshindi wa juu atatokana na kundi la Halmashauri za wilaya na atapata zawadi ya Shilingi Milioni Hamsini.

Hata hivyo, Dkt. Ndugulile ametoa wito kwa Halmashauri zote nchini kuiga mfano wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ambayo imewezesha kaya zake zote kuwa na vyoo bora. Naibu Waziri amesema usafi wa mazingira na matumizi ya vyoo bora unaweza kupunguza magonjwa ya kuambukiza kwa zaidi ya asilimia 80 na hivyo kuipunguzia serikali gharama za kununua madawa na kupambana na magonjwa ya milipuko.

Chanzo: Blog ya Wizara ya Afya (afyablog.moh.go.tz)


Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.