MKUU wa Mkoa wa Dodoma Rosemary Senyamule ameipongeza Shule ya vipaji maalumu ya Sekondari ya Wasichana ya Msalato Mkoani Dodoma kufuatia matokeo mazuri ya kidato cha Sita kwa kupata ufaulu wa alama ya daraja la kwanza 139 na 6 kwa daraja la pili.
Pongezi hizo alizitoa wakati ya ziara yake ya kikazi ya kukagua hatua ya ujenzi wa mabweni manne, vyumba saba vya madarasa na matundu 10 ya vyoo katika shule hiyo na Shule ya Sekondari Bihawana ambapo ujenzi wa matundu sita ya vyoo, bweni moja na vyumba vinne vya madarasa chini ya fedha kutoka serikali kuu. Katika shule ya Sekondari Msalato awamu ya kwanza ilipokea kiasi cha Shilingi Milioni 428 na awamu ya pili shilingi milioni 260 ikiwa ni nyongeza kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopangwa kuhitajika mabweni mawili ya ziada na Sekondari ya Bihawana shilingi milioni 227.2
"Nichukue nafasi hii kuwapongeza walimu na wanafunzi kwa kuufaharisha Mkoa wetu wa Dodoma, tunatamani kila mtu anaefanya kazi Mkoani hapa aifaharishe kwa nafasi yake kama hivi mlivyo fanya ninyi hongereni sana mmetupa heshima kubwa sana na nimategemeo yetu kuwa mtaendelea kufanya vizuri zaidi", alieleza Senyamule
Awali, Senyamule alikagua ujenzi unaoendelea shuleni hapo na kuwaasa wakandarasi wanaosimamia miradi kuhakikisha wanaongeza kasi ya umaliziaji wa miradi hiyo kwa viwango vinavyotakiwa kwa kuzingatia muda uliobaki ili wanafunzi wa kidato cha tano wanapoingia waweze kutumia miundombinu hiyo, ikiwa imekamilika kwa ubora unaotakiwa.
"Lazima siku zilizobaki mjitahidi kuongeza kasi na kuongeza ubunifu ili kuendana na wakati uliobaki kwa kuzingatia ubora unaotakiwa, ongezeni idadi ya mafundi na ongezeni masaa ya kufanya kazi, hapa inahitajika "speed and accuracy" bahati nzuri hapa umeme upo tumieni nafasi hii kukamilisha kazi hii" alisisitiza Senyamule
Akiwa katika Shule ya Sekondari ya Bihawana Mkuu wa Shule hiyo Mwalimu Liberatus Ntilema amesema ujenzi katika Shule hiyo uko katika hatua za ukamilishaji na mkakati uliopo ni kukamilisha mradi huo wa ujenzi ifikapo tarehe 30/07/2023.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.