• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

Serikali yajizatiti kuendeleza kilimo cha zao la zabibu

Imewekwa tarehe: August 13th, 2021

WAZIRI Mkuu Kassim Majaliwa amesema Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuendeleza kilimo cha zao la zabibu na kuhakikisha linaleta tija kwa wakulima.

Ameyasema hayo Ijumaa Agosti 13, 2021 alipotembelea mashamba ya zabibu ya Chinangali na Bihawana akiwa katika muendelezo wa ziara zake za kukagua maendeleo ya zao hilo.

Aidha, Waziri Mkuu amewashauri wakulima watenge sehemu ya mashamba yao na kulima zabibu za mezani ambazo nazo zina faida kubwa badala ya kulima za kuzalisha mvinyo tu.

Pia Waziri Mkuu amemuagiza Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Joseph Mafuru ahakikishe anaandaa utaratibu wa kusasaidia wakulima wa zabibu wa Bihawana kwa kuwawekea mfumo wa umwagiliaji.

Waziri Mkuu amesema zabibu zinazopatikana mkoani Dodoma zina thamani kubwa na ni nzuri kwa utengenezaji wa mvinyo ukiliganisha na zabibu zinalizomwa katika maeneo mengine.

Amesema kilimo hicho kinwamuwezesha mwananchi kuboresha uchumi wake, hivyo amewashauri wakazi wa mkoa wa Dodoma wakiwemo watumishi wa umma wachangamkie fursa hiyo.

Waziri Mkuu ametumia fursa hiyo kuwahakikishia wakulima wa zabibu kwamba Serikali imedhamiria kuboresha kilimo cha zao hilo kwa sababu kilimo ni mkombozi kwa Watanzania.

Wakulima wasaidiwe kuanzia hatua za awali za uandaaji wa mashamba, upatikanaji wa mbegu, pembejeo hadi hatua ya utafutaji wa masoko.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema wizara hiyo ipo katika mkakati wa kufufua shamba la zabibu la Chinangali na tayari wameanza na ukarabatti wa mfumo wa maji.

Amesema wamefanikiwa kufufua visima vitatu ambavyo vinapeleka maji katika bwawa la umwagiliaji na kwamba wanatarajia kuweka upya mfumo wa umwagiliaji katika shamba lote.

Waziri huyo amesema hatua hiyo inatokana na kuharibika kwa mfumo wa awali wa umwagiliaji uliokuwa umefungwa kwenye shamba hilo. Shamba la Chinangali lina ukubwa wa ekari 600 na kati ya hizo, ekari 300 ndizo zimeendelezwa.

Pia, Waziri huyo amesema mbali na kufunga upya mfumo wa umwagiliaji, pia wameweka lengo la kuzalisha miche 500,000 kwa ajili ya kupanda upya shamba hilo.

“Kituo cha TARI Makutupora kimeotesha miche mingi ya zabibu za mezani ambayo itagawiwa kwa wakulima ili waweze kupanda kuzalisha aina hiyo ya zabibu kwa wingi” alisema Bashe.

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiangalia zao la zabibu shambani.



Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa Ofisi ya Waziri Mkuu (owm_tz)

Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Barabara ya Lami ya Kilometa 6 yawanufaisha wakazi wa Kata ya Miyuji

    April 23, 2025
  • Huduma ya Chakula na Lishe yapandisha ufaulu Shule ya Sekondari Nala

    April 22, 2025
  • Mradi wa Maji Nala wa Bil. 1.3, mkombozi kwa wananchi

    April 22, 2025
  • Milioni 500 kukamilisha mradi wa Kituo cha Afya Kizota

    April 22, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.