Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbas amewataka Waandishi wa Habari nchini kutekeleza majukumu yao kwa weledi ili kuepuka makosa ya kisheria yanayoweza kujitokeza.
Dkt. Abbas ameyasema hayo leo jijini Dodoma alipokuwa akitoa mada juu ya “Matumizi ya Mitandao ya Kijamii” wakati wa mafunzo kwa waaandishi wa Habari za mtandaoni wa Shirika la Utangazaji Tanzania – TBC, (TBCOnline).
Amewataka kutojiona wanyonge kwa kufanya kazi hiyo, bali wajione watu waliobeba dhamana kubwa katika kuihabarisha jamii mambo mbalimbali yanayoendelea duniani.
“Si lazima waandishi wote wa Habari waonekane kwenye Televisheni, kuna namna nyingi za kufanya kazi hii ikiwemo mitandao ya kijamii ambayo watumiaji wake wanaongeneza kwa kasi, kwa sasa dunia imehama kutoka mtaani kwenda mtandaoni.” Amefafanua Dkt. Abbas.
Mafunzo haya ni muendelezo wa mafunzo ya siku 4 kwa wanahabari hao ili kuwajengea uwezo Zaidi kuhusiana na mitandao ya kijamii.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.