MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mh. Anthony Mavunde leo amezindua mradi wa Saluni kikundi cha Vijana kiitwacho UBINADAMU KAZI kilichopo kata ya Matukupora Jijini Dodoma na kuwapongeza kwa kukamilisha saluni 6 za kiume na kike.
Mbunge Mavunde amewapongeza Vijana hao kwa kujituma na kufanya kazi kwa bidii mpaka kufikia hatua ya umiliki wa saluni 6, na ametumia fursa hiyo kuwataka Vijana wengine kuiga mfano huo mzuri na kujiunga katika vikundi ili waweze kupatiwa mikopo.
Akijibu risala ya Kikundi hicho, Mbunge Mavunde amewaahidi vijana hao kuwatafutia maeneo ya kujenga majengo ya kudumu na pia amewachangia shilingi 1,000,000 kwa ajili ya uendeshaji wa miradi yao.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.