MBUNGE wa Jimbo la Dodoma Mjini Mhe. Anthony Mavunde amekutana na kuzungumza na wazazi/walezi pamoja na watoto wenye mahitaji maalum leo katika Kata ya Nghongh’ona baada ya kukabidhi viatu vya shule kwa watoto 28.
Aidha, Mbunge Mavunde ameahidi kuwalipia bima ya Afya watoto wote, kutoa madaftari 300 pamoja na masweta 28 ya shule kwa ajili ya watoto hao wanaosimamiwa chini ya Taasisi ya The Best Child Care Foundation.
Zoezi hilo la ugawaji wa viatu limehudhuriwa na uongozi wa Kata ya Nghongh’ona wakiongozwa na Diwani Mhe. Loth H. Loth.
Mbunge wa Jimbo la Dodoma Mhe. Anthony Mavunde (aliyesimama) akizungumza na watoto, walezi na wazazi wa watoto wenye mahitaji maalum katika eneo la Nghong'ona (kulia ni diwani wa kata ya Nghong'ona Mhe. Loth Loth .
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.