• Wasiliana nasi |
    • Maswali na majibu |
    • Baruapepe - Watumishi |
    • eVibali |
    • Malalamiko |
Dodoma City Council
Dodoma City Council

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Jiji la Dodoma

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya
      • Fedha na Biashara
      • Elimu ya Msingi
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Mifugo na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii, Ustawi wa Jamii, Jinsia na Vijana
      • Ujenzi
      • Mazingira na Udhibiti wa Taka ngumu
    • Vitengo
      • Sheria na Usalama
      • Mkaguzi wa Ndani
      • TEHAMA na Uhusiano
      • Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuji
    • Ward
  • Fursa za Uwekezaji
    • Maeneo ya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Mji wa Serikali
    • Kwa nini uwekeze Dodoma?
  • Huduma Zetu
    • Maendeleo ya jamii
    • Elimu
    • Miundombinu
    • Mazingira
    • Afya
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Fedha na Utawala
      • Mipango miji na Mazingira
      • Uchumi, Afya na Elimu
      • Kudhitibi UKIMWI
      • Maadili
    • Kamati zingine/Bodi/Uwakilishi
    • Ratiba
      • Vikao vya Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi itakayotekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Ripoti
    • Sheria Ndogo
    • Miongozo
    • Mpango Mkakati
    • Fomu
    • Jifunze Nyumbani
    • Mpango Kabambe
    • Jarida
    • Asemavyo Mahia - Afya na Mazingira
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya picha
    • Habari
    • Matukio
  • City TV

MAWAKILI NCHINI WATAKIWA KWENDA KUZISOMA SHERIA ZA UCHAGUZI MKUU

Imewekwa tarehe: July 2nd, 2025

Na. Janeth Raphael MichuziTv -Dodoma

Mawakili nchini Tanzania wametakiwa kwenda kuzisoma sheria za Uchaguzi Mkuu, ili waweze kuwasaidia kujaza fomu wagombea waliojitokeza kutia nia, lakini pia kutatua migogoro itakayowasilishwa kwa kukosa uelewa katika Mahakama mbalimbali hapa nchini.


Jaji Mkuu wa Tanzania ,George Masaju aliyasema hayo jijini Dodoma wakati akiwathibitisha na kuwapokea Mawakili 449 wakiwemo wa Serikali na wa kujitegemea, ikiwemo kuorodheshwa rasmi katika orodha ya mawakili waliothibitishwa hapa nchini.


Aidha, aliwataka Mawakili hao kwenda kufanya kazi katika mikoa mingine tofauti na Dar es Salaam na Dodoma ambayo ina mawakili wa kutosha, ili kuepuka kuitwa vishoka hasa ukizingatia soko la Kada hiyo ni kubwa kwa sasa.

Alisema kuwa kuna sheria nyingi zikiwemo za Polisi, Uchaguzi na nyingine. Na kusema kuwa Mawakili wanapaswa kutumia muda mwingi kuzisoma na kuzielewa ili waweze kutumia fursa ya kuwasaidia wagombea mbalimbali waliojitokeza kuchukua fomu za kugombea nafasi za uongozi. “Najua kazi zetu nyingi tunazipata kupitia kutatua migogoro mbalimbali. Hivyo, tuweke jitihada ya kuzisoma sheria ili tuzielewe maana kuthibitishwa, kupewa vyeti na utendaji ni vitu viwili tofauti” alisema Jaji Mkuu Masaju.

Vilevile, aliwataka Mawakili kwenda kukiishi kiapo walichoapa na kukifanyia kazi ipasavyo, wasome sheria kila mara kwa sababu hubadilika, ili waweze kuisaidia jamii kwa ujumla katika maeneo ambayo watakwenda kuwajibika hapa nchini. “Sisi tuliojaa hapa wakati mnapewa kiapo hatujaja kuwashangilia tumekuja kushuhudia kiapo chenu kama mtakwenda kukiishi kama Sheria inavyoelekeza” alisema.

Jaji Mkuu akizungumzia kuhusiana na Mawakili hao kupenda kuishi kwenye miji mikubwa kama Dar es Salaam na Dodoma, alisema kitendo hicho kinamchukiza sana kwa sababu kuna maeneo mengi ambayo yana migogoro na kuwataka waende sehemu hizo wakawatumikie wananchi.

Akitolea mfano Wilaya ya Kilombero ambako kuna mashamba ya miwa, kuna wakulima wengi pamoja na jamii ambayo inahitaji huduma ya sheria, hivyo, waende huko kuwatumikia wananchi badala ya kubaki kwenye miji mikubwa. “Nisingependa kuona mnazunguka Dar es Salaam na Dodoma muonekane kama vishoka, tawanyikeni mikoa mingine mkafanye kazi ya kutenda haki ili kuisaidia jamii, lakini sitaki kusikia mnauza utu wenu kwa kupewa fedha badala ya kutenda haki” alisema Jaji Mkuu.

Alisema kuwa wasitegemee kwenda kuishi kama wanasiasa wao wanapaswa kwenda kutenda haki ili kuendelea kuaminika mbele ya jamii na kuongeza kuwa kama kesi haiwezi anapaswa kumwambia mteja wake ukweli na sio kuchukua pesa yake bure. “Msitende dhambi ya kuchukua fedha ya watu ilihali mnajua kesi huiwezi ni bora umwambie ukweli mteja, usiwaze kununua gari ndogo kwa pesa ya mteja ambayo unajua kesi hashindi, hata wewe hutafanikiwa kwa sababu hujui amehangaika vipi kuitafuta hiyo pesa ili akulipe” alisema.

Naye Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Chiganga Tengwa alisoma idadi ya mawakili waliopokelewa na kuthibitishwa huku akiwataka kufuata taratibu watakazoelekezwa.

Ongezeko la idadi hiyo ya Mawakili waliothibitishwa imefanya kufikia mawakili 13,446 ambao watakuwa wanafanya shughuli za uwakili katika maeneo mbalimbali hapa nchini.



Matangazo

  • MKUTANO WA BARAZA LA WAHESHIMIWA MADIWANI January 30, 2025
  • KITUO CHA AFYA ILAZO KIMEANZA KUTOA HUDUMA January 13, 2025
  • HOSPITALI YA JIJI LA DODOMA IMEANZA KUTOA HUDUMA ZA AFYA January 12, 2025
  • TANGAZO LA UUZWAJI WA VIWANJA KIKOMBO December 03, 2024
  • Angalia zote

Habari za hivi punde

  • Serikali yaboresha mazingira ya kufundishia na kujifunza- Mwambene

    August 18, 2025
  • Afisa elimu mkoa wa Dodoma akagua maandalizi ya Juma la elimu ya watu wazima

    August 17, 2025
  • Wafanyabiashara wa mkoa wa Dodoma watangaziwa fursa za biashara nchini indonesia

    August 16, 2025
  • Wafugaji waaswa kufuga kwa kuzingatia uwezo wa malisho ili kupata tija

    August 15, 2025
  • Angalia zote

Video

Watendaji Kata Wilaya ya Dodoma watakiwa kusimamia maswala ya Lishe
Video zaidi

Viunganishi vya Haraka

  • Historia ya Manispaa
  • Wasifu wa Manispaa
  • Kata na Madiwani
  • Mji wa Serikali
  • Orodha ya Madiwani
  • Mpango Mkakati wa Halmashauri (SP)
  • Kwanini uwekeze Dodoma?
  • Zabuni za Wakala wa Ukusanyaji Mapato
  • Zabuni ya Usafi wa Mazingira

Viunganishi Linganifu

  • Msalato Sekondari
  • Mkoa wa Dodoma
  • OR-TAMISEMI
  • Utumishi
  • Chuo Kikuu Dodoma (UDOM)
  • Bunge

World visitors tracker

world map hits counter

Idadi ya watembeleaji

free HitCounter

Ramani elekezi

Wasiliana nasi

    1 CDA Street, 40477

    Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA

    Simu: +255 26 232 4817

    Simu ya kiganjani:

    Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya tovuti

Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.