Na. Dennis Gondwe, DODOMA
KWAYA ya UMISSETA Dodoma mwaka 2021 imeahidiwa kurekodiwa wimbo wao wa kuusifia Mkoa wa Dodoma katika studio ya kisasa ili kuuongezea thamani na kuwafikia watu wengi zaidi.
Ahadi hiyo imetolewa na Mbunge wa Jimbo la Dodoma mjini, Anthony Mavunde katika hafla fupi ya kukabidhi ‘tracksuit’ 100 kwa wanamichezo wanaoshiriki UMISSETA Jiji la Dodoma tukio lililofanyika katika ukumbi wa shule ya sekondari ya Dodoma leo mchana.
Mbunge Mavunde amesema “kwaya hii imeimba vizuri sana. Nawapa ofa ya kuwarekodia wimbo wenu studio ya kisasa. Sisi ni jiji ambalo ni makao makuu ya nchi. Lazima mambo yenu yawe tofauti na makubwa” amesema Mavunde. Aidha, ameahidi kuwatengenezea sare za kisasa ili wapendeze zaidi waimbaji hao.
Michezo ya UMITASHUMTA na UMISSETA mwaka 2021 inaongozwa na kaulimbiu isemayo “Michezo, Sanaa na taaluma kwa maendeleo ya viwanda”.
1 CDA Street, 40477
Anuani ya posta: 1249, DODOMA, TANZANIA
Simu: +255 26 232 4817
Simu ya kiganjani:
Baruapepe: cd@dodomacc.go.tz
Copyright ©2017 The City Council of Dodoma. All rights reserved.